May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar yapiga ‘stop’ disko toto

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limepiga marufuku disko toto katika kumbi zote za starehe mkoani humo, wakati wa sherehe za sikukuu ya Eid El-fitri. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Jeshi hilo kwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vimejipanga kikamilifu kuimarisha usalama katika kipindi cha sikukuu hiyo inayotarajiwa kuadhimishwa kesho au keshokutwa Ijumaa, tarehe 14 Mei 2021.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 12 Mei 2021 na Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, wamejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, fukwe za bahari, kumbi za starehe na maeneo mengine yote yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu.

Pia, wazazi wahakikishe watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu na kutowaruhusu kuogelea peke yao, kitendo ambacho kinaweza kuzuia watoto hao kuzama kwenye maji.

“Wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo,” amesema

Mambosasa, amewataka madereva wa vyombo vya moto wanatakiwa kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha magari au pikipiki wakiwa wametumia vilevi/pombe.

error: Content is protected !!