May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar yakamata 31 tuhuma ‘panya road’

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es limesema limefanikiwa kuwakamata watu 31 kwa tuhuma za unyang’anyi, kujeruhi na kupora maarufu kama ‘Panya road.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi tarehe 7 Mei 2022 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, ACP Muliro J. Muliro imeeleza kuwa kukamatwa huko ni kufuatia operesheni maalumu na msako wa mtaa kwa mtaa dhidi ya panya road.

Amesema wengi wa wahalifu hao ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 13-20 ambao hutumia mapanga, visu, nondo, na mikasi mikubwa kufanya uhalifu huo.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kushirikiana na raia wema kw akupokea taarifa mbalimbali za wahalifu na linaahidi kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwakamata kabla ya kutena uhalifu,” amesema Muliro.

Ameongoeza kuwa katika mahojiano ya kina Jeshi la Polisi limebaini kuwa watuhumiwa hao wamehusika katika vitendo hivyo vya kihalifu na kuonesha baadghi ya vitu walivyoiba ikiwemo TV 12 na simu nne.

Amesisitiza jeshi la polisi halitasisita kuwakamata ambao wamekuwa wakipokea mali mbalimbali za wizi zinazotokana na matukio yakihalifu.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limemkamata Fakhi Hamisi (30) mkazi wa Ununio na wenzake 33 wakiwa na bhangi magunia 10 yenye uzito wa kilo 180, kete 497 na puli 48.

Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa huyona wenzake walikamatwa maeneo ya Kinondoni baada ya jeshi la polisi kupata taarifa fiche za kihalifu.

“Watuhumiwa hawa walikutwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania pea moja, darubini, kisu, blanketi na viatu mbalimbali vya Jeshi pamoja na pikipiki sit ana bajaji moja mali ambazo ni zao matokeo ya kazi za kihalifu toka kwa raia wema walioporwa,” amesema.

error: Content is protected !!