August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar wamuua jambazi

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemuua mtu anayesadikiwa kuwa jambazi, na kwatia nguvuni watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni vinara wa wizi wa magari, anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na wandishi wa habari leo hapa jijnini Simon Sirro, Kamishina wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amesema kuwa mpaka sasa jeshi hilo halijapata jina kamili la mtuhumiwa wa ujambazi aliyeuawa.

“Mnamo Julai 26 mwaka huu kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kilifanya msako maeneo ya Masaki barabara ya Msasani na kufanikiwa kumuua jambazi mmoja hatari   na kumnyang’anya bastola aina ya Glock 17 ikiwa na risasi sita,” amesema Sirro na kudai;.

Hapo awali mtu huyo alikuwa akifukuzwa pamoja na wenzake wawili, lakini akatoa bastola ili kukabiliana na askari ndipo polisi walipomfyatulia risasi iliyomjeruhi na kumsababishia kifo.

Pia Kamanda Sirro amesema jeshi la polisi limekamata watu wawili wanaotuhumiwa kuwa vinara wa wizi wa magari.

“Watuhumiwa tuliowakamata ni Rauben Kabamba ambaye ni dalali wa magari na mkazi wa Mbezi na Alpha Lymo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha mkoani Pwani,” amesema.

Aidha, Kamanda Sirro amesema jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa wawili waliokutwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Watuhumiwa hao ni Dikson Mtalemwa (27) na Manase Yohana (27). Huu ni muendelezo wa ripoti za utendaji wa kila wiki wa jeshi la polisi ambazo hutolewa na kamanda Sirro makao makuu ya jeshi hilo, kanda maalum ya Dar es Salaam.

error: Content is protected !!