June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi Dar ‘wadhulumiwa’ posho

IGP, Ernest Mangu

Spread the love

ASKARI wa Jeshi la Polisi wapatao 50 Jijini Dar es Salaam wameulalamikia uongozi wa jeshi hilo kwa kuwapiga danadana kuhusiana na posho zao walizoahidiwa kutokana kushiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Madola, uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Wakizungumza na mwandishi wa MwanaHalisionline aliyekuwepo eneo la tukio kwa masharti ya kutotajwa majina yao baadhi ya askari hao wamesema mkutano huo uliaanza julai 13 na unamalizikia leo na walitakiwa kulipwa posho kimafungu kulingana na madaraja yao.

Wamesema kundi la kwanza linatakiwa kulipwa posho y ash.300,00, kundi la pili ni wale waliopangwa kulinda katika mahoteli wanatakiwa kulipwa sh.250,000 na wanaoshiriki kwenye mkutano huo wanatakiwa kulipwa sh.200,000.

Aidha, wamesema kuwa walipompigia simu kiongozi wao waliyemtaja kwa jina la Ispekta Nyangogo kudai posho zao  aliwaambia waende ofisini kwake lakini walipoenda wawakilishi wao walijibiwa kuwa hawalipwi na waende kushitaki kokote wanakotaka.

Hata hivyo Inspekta  Nyagongo alipotafutwa kwa njia ya simu alijibu kuwa yeye hahusiki na kumtaka mwandishi awatafute Kamanda Nyambabe na Muhume kuzungumzia suala hilo ambao alidai ndio  wahusika.

Kamanda Nyambabe hakupatikana alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi, lakini Kamanda Muhume aliopotafutwa amesema askari hao wanatakiwa kufuata taratibu kudai posho zao na sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu.

Kamanda Muhume amesema jeshi hilo halihusiki kulipa posho hizo na kuwataka waende utumishi kupitia kwa Katibu Mkuu wao ili walipwe madai hayo.

error: Content is protected !!