Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar mguu sawa sikukuu ya Eid
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar mguu sawa sikukuu ya Eid

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewahakikishia  hali ya usalama na amani wakazi, wananchi wa jiji la Dar es Salaam katika kipindi chote cha sikukuu ya Eid inayotarajiwa kuwa kati ya Jumapili wiki hii au Jumatatu ijayo, anaandika Yasinta Francis.

Lucas Mkondya, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema kuwa askari wa jeshi hilo wamejipanga vyema kuhakikisha wananchi wa jiji la Dar es Salaam wanasherehekea sikukuu hiyo kwa kwa amani na utulivu pasipo bugudha za wahalifu.

“Uzoefu unaonesha kuwa, mara nying kipindi cha sikukuu kama hii watu wenye nia ovu hujiandaa kufanya vitendo vya kihalifu, ndiyo maana tumejipanga kukabiliana na aina yoyote  ya uhalifu kwa kuzuia au kuwatia nguvuni wote watakaoshiriki vitendo vya uvunjifu wa sheria,” amesema.

Kamanda Mkondya amesema polisi watafanya doria za masaa 24 katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam hasa maeneo yenye korofi na yenye rekodi au viashiria vya uhalifu.

“Pia kutakuwa na doria katika maeneo ya misikiti, kumbi za starehe na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na tutatumia taarifa za kiintelijensia ili kuwabaini wahalifu wanaopanga kufanya matukio ya uhalifu.

“Tutaimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuhakikisha maeneo yote hatarishi yanadhibitiwa,” amesema Kamanda Mkondya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!