October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi aliyemuua George Floyd akata rufaa

Spread the love

 

DEREK Chauvin (46), aliyekuwa askari polisi wa mji wa Minneapolis, Jimbo la Minnesota nchini Marekani, anayetumikia kifungo cha miaka 22 na nusu gerezani, amekata rufaa kupinga kifungo hicho. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Chauvin alianza kutumikia kifungo hicho, tarehe 25 Juni 2020, baada ya Mahakama ya Minnesota mbele ya Jaji Peter Cahill kumkuta na hatia ya mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd.

Mauaji hayo aliyoyafanya tarehe 25 Mei 2020 kwa kumbana shingoni kwa takribani dakika 10 na kumfanya Floyd kushindwa kupumua, yalisababisha maandamano nchini humo ili kukomesha ukatili unaofanywa na polisi dhidi ya watu weusi.

Adhabu hiyo ya miaka 22 na nusu ilielezwa kuwa ni ndogo tofauti na kifungo cha miaka 30 walichokuwa wanakitaka upande wa mashtaka.

Akiendelea kutumikia adhabu hiyo, juzi Alhamisi tarehe 23 Septemba 2021, Chauvin anayeelezwa kuwa mzungu wa kwanza kuwajibishwa kwa kumuua Mmarekani mweusi amewasilisha rufaa yenye hoja 14 ikiwa ni siku mwisho ya kukata rufaa kwa mujibu wa sheria.

Alikata rufaa juu ya hukumu hiyo Alhamisi usiku mbele ya mahakama ya wilaya ya Minnesota, siku ya mwisho, ambayo aliruhusiwa kufanya hivyo, kwa mujibu wa sheria.

Miongoni mwa hoja hizo, anapinga jopo lililochaguliwa kusikiliza kesi hiyo.

error: Content is protected !!