Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili
Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love

 

MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi, Fredrick Ole Leliman kwa mauaji ya wakili Willie Kimani na wengine wawili yaliyotokea mwaka 2016. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Maiti za watatu hao zilipatikana zikiwa zimeshindiliwa kwenye mifuko ya plastiki na kutupwa mtoni katika kaunti ya Machakos nchini humo.

Ifahamike kuwa hukumu ya kifo ilitekelezwa kwa mara ya mwisho miaka 30 iliyopita japo bado adhabu hiyo inaendelea kutolewa.

Baada ya miaka isiyopungua sita, hatimaye familia ya wakili Willie Kimani sasa inashusha pumzi baada jana watuhumiwa katika kesi hiyo kupatikana na hatia.

Jaji Jessie Lessit wa mahakama ya rufaa, aliwatia hatiani na kumhukumu kifo afisa wa polisi Fredrick Ole Leliman kwa mauaji ya wakili huyo na wengine wawili ya mwaka 2016.

Afisa wa polisi Stephen Cheburet naye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, mwenzake Sylvia Wanjiku miaka 24 jela wakati Peter Ngugi aliyekuwa msaidizi akifungwa miaka 20 jela.

Watatu hao walitiwa hatiani mwezi Julai mwaka uliopita wa 2022. Jaji Jessie Lessit aliwapata na hatia ya mauaji ya mtetezi wa haki za binadamu Willie Kimani na mteja wake Josephat Mwenda pamoja na dereva wa teksi Joseph Muiruri waliopoteza maisha tarehe 23 Juni mwaka 2016.

Rebecca Mwenda ambaye ni mjane wa marehemu Josephat Mwenda, alidondoka na kuzirai alipojaribu kuzungumza na waandishi wa habari baada ya hukumu kutangazwa.

Kwa upande mwingine mahakama iliipa uzito hoja kuwa ushuhuda wa Peter Ngugi uliwasaidia jopo la wachunguzi.

Ushuhuda wake ndio uliomnasa afisa Fredrick Leliman kwani alikiri na kuwaelezea wachunguzi kuwa Willie Mwenda na Muiruri waliuawa kinyama.

Kufuatia hilo, Peter Ngugi aliiomba mahakama asihamishiwe jela nyengine kwa kuhofia usalama wake.

Amekuwa akizuiliwa kwenye jela ya Naivasha wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea na anaripotiwa kubadili mienendo na kuwa mcha Mungu sasa ni kasisi.

Aidha, Cliff Ombeta ambaye ni wakili wa maafisa wa polisi Fredrick Ole Leliman na Steven Chebureti ametangaza kuwa atakata rufaa.

Ifahamike kuwa Kenya ilitekeleza kwa mara ya mwisho hukumu ya kifo zaidi ya miaka 30 iliyopita ijapokuwa bado inaendelea kuitoa adhabu hiyo. Mwaka 2017, mahakama ya juu iliamuru kuwa hukumu ya kifo ya inakiuka katiba.

Ripoti mpya ya mradi wa hukumu ya kifo kutoka Ofisi ya Mashtaka ya Serikali ya Kenya kwa ushirikiano na tume ya taifa ya kutetea haki za binadamu (KNCHR), jumla ya wafungwa 600 wamehukumiwa kifo na wanasubiri adhabu hiyo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi,...

Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza...

Kimataifa

Magharibi kuwekeza silaha Indo-Pacific, China yachochea

Spread the love KUVUNJIKA ushirhikiano wa China na Magharibi uliodumu kwa takribani...

Kimataifa

Ruto amlaumu Odinga kujaribu kuanzisha mgogoro kwa mara ya pili

Spread the love  RAIS wa Kenya William Ruto amesema kwamba hatakubali “kutoijali...

error: Content is protected !!