Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi, ACT-Wazalendo wavimbiana
Habari za Siasa

Polisi, ACT-Wazalendo wavimbiana

Spread the love

JESHI la Polisi nchini, limekataza kufanyika maandamano ya tarehe 9 Aprili 2019 yaliyopangwa na Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wakati jeshi hilo likikataza maandamano hayo, ACT-Wazalendo wameeleza kuwa, watafanya kwa kuwa ni haki yao ya kikatiba.

Tarehe 6 Aprili 2019 Isack Nyasilu, Katibu wa Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo, alitangazakufanya maandamano kesho tarehe 9 Aprili, 2019 kupinga azimio la bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Taarifa hiyo ya zuio la polisi imewekwa leo tarehe 8 Aprili 2019 katika ukurasa wake wa Twitter wa ACT-Wazalendo ikieleza kuwa, polisi wamepiga marufuku maandamano hao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amezuia maandamano hayo.

Licha ya zuio hilo, Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo imesema, utaratibu wake katika kushiriki maandamano hayo uko pale pale.

“Tumepokea taarifa RPC wa Dodoma kuwa amezuia maandamano ya Ngome, Jumuiya na Mabaraza ya Vijana ya Vyama vya siasa.

“Tunapenda kumjulisha kuwa, sisi kama Social Auditors tunahaki ya kuhoji na kusimama na CAG, tunaendelea na maandamano kama yalivyopangwa kwa kuwa, ni haki yetu ya kikatiba,” inaeleza taarifa ya Ngome ya Vijana ya ACT-Wazalendo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, utaratibu wa usafiri wa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Singida na Iringa kwenda Dodoma kushiriki maandamano ya tarehe 9/4/19 upo kama ulivyopangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!