Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole: Viongozi wasioridhika, tosheka hawafai
Habari za Siasa

Polepole: Viongozi wasioridhika, tosheka hawafai

Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, amesema viongozi wa umma wasioridhika na nyadhifa zao, hawana nafasi ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma…(endelea).

Polepole ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 18 Julai 2020, wakati akizungumza katika mkutano wa kuelezea utekezaji wa Ilani ya CCM, katika Mkoa wa Ruvuma.

Kauli hiyo ya Polepole imekuja katika kipindi ambacho kuna wimbi la wateule wa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kuomba likizo kwa ajili ya kujitosa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa Oktoba 2020.

Katika nyakati tofauti, Rais Magufuli aliwasihi wateule wake kuridhika na kutosheka na nyadhifa zao. Kauli hiyo ilisisitizwa pia na makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Licha ya kwamba Polepole hakuweka bayana viongozi hao wa umma hawaridhiki kivipi, katibu huyo wa uenezi amesema CCM inawasubiri kuwaona wakati wa uteuzi huku akiwapongeza viongozi wa kuteule Mkoa wa Ruvuma kwa kutokuondoka.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Soma zaidi hapa

JPM: Sijamtuma mtu akagombee, awapa ujumbe wanaCCM

“Mmeona kwenye safu ya serikali kuna mtu ameondoka? Ni vizuri tukasema Rais alipovuka uchaguzi wa 2015 aliwaita njoo shika nafasi hii nisaidie, unafika mtoni unamwambia mi siendi, kavuka mwenyewe, nii ulaghai huu,” amesema Polepole.

Huku akishangiliwa, Polepole amesema, “haiwezekani kuondoka hivihivi, mi nawapongeza safu ya viongozi wakuu wa mikoa na wilaya Ruvuma, ninyi Mungu amewasaidia mmeona mbele. Tunasubiri sisi hatusemi lolote.”

Polepole amesema, viongozi hao na wasiotosheka na kazi wanazopewa hawaaminiki.
“Viongozi wasiotosheka ni shida, hawataaminika popote. Mtu asiyetosheka ukimpa kazi hii atakuacha atachukua nyingine, hatatosheka atakuacha mtoni, hii mambo ya kuachana mtoni mwenyekiti (Rais Magufuli) anatusaidia anaanza kuiweka sawa,” amesema Polepole

Soma zaidi hapa

Ubunge CCM: ‘Wateule wa Rais’ wachongewa CDF na Samia watoa neno

“Wewe si unakwenda? Tuachie mambo yetu uende, kenye chama nisiwaambie lakini ukweli…., umeenda (Rais Magufuli) anakuachia uende, lakini kwa kweli mtu aliyekusaidia mtoni usimkimbie.”

Jana Ijumaa saa 10 jioni, ndiyo ilikuwa mwisho wa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho kiwateue wana CCM kugombea udiwani, ubunge na uwakilishi.

Baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya, katibu tawala wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, mashirika ya umma pamoja na makatibu wakuu wameziacha nafasi zao na kwenda kugombea na nafasi zao Rais Magufuli amewateua wengine.

Tarehe 20 na 21 Julai 2020 itakuwa ni mikutano mkuu ya majimbo na wilaya kupiga kura za maoni za wagombea wa ubunge na ujumbe wa baraza la wawakishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!