May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polepole: JPM hatoongeza muda, itabaki hivyo

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Spread the love

HUMPHREY Polepole, mbunge wa kuteuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema mwenyekiti wake Rais John Magufuli hatoongeza muda madarakani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma.

Akizungumza bungeni leo tarehe 9 Febrari 2021, Polepole amesema ndani ya chama chao wameelezwa, na kwamba itabahi kivyo hivyo, hakuna wa kubadilisha.

“Rais hataongeza muda,” amesema Polepole na kuongeza “sisi ndani ya chama tulishaelezana. Yeye (Rais Magufuli) ndiyo msemaji mkuu.”

Polepole ametoa kauli hiyo ikiwa tayari joto la kauli za kutaka Rais Magufuli aongezewe muda likianza kupanda.

Hivi karibuni, baadhi ya wanasiasa wamenukuliwa wakitaka Rais Magufuli aongezewe muda wa kusalia madarakani zidi kwa madai, amefanya kazi iliyotukuka.

Rais John Magufuli

Joseph Msukuma ambaye ni Mbunge wa Geita Vijijini alilitaka Bunge kuangalia uwezekano wa kumwongezea rais muda wa kuongoza, alimtaka Rais Magufuli kuanza kufikiria hilo.

“Tumeanzisha miradi mikubwa kwa ujasiri wa mtu mmoja, na hakuna ubishi kwamba bila Magufuli (Rais Magufuli) mawazo yake yale, tusingefika hapa tulipo.

“Haya mambo ambayo rais ameyafanya kwa ujasiri ule ule, tunaweza kuona namna kama alivyosema Mzee Butiku juzi, tukamuongeza muda kwani kitu gani? mbona wenzetu wamefanya,” alisema Msukuma.

Kabla ya Msukuma, Mze Butiku alieleza kwamba, haoni tatizo lolote kwa kuwa, mataifa mengine yamefanya hivyo kwa watawala wao kuwepo madarakani muda mrefu.

“Mbona Waingereza wazungu wameongoza miaka mingi, masultani haya wameendesha nchi zao miaka mingi, nani aliwauliza, waongo tu,” alisema Butiku tarehe 6 Februari 2021, katika Maadhimisho ya Miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma.

error: Content is protected !!