May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polepole, Askofu Gwajima njiapanda CCM

Askofu Josephat Gwajima

Spread the love

 

WAKATI chanjo ya kinga ya ugonjwa wa korona (Uviko-19) ikiendelea kutolewa nchini Tanzanioa, wabunge wawili wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameweka msimamo wa kutokubaliana na chanjo hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wabunge hao ambao wamejitokeza kwenye mikusanyiko ya hadhara na mitandao ya kijamii ni Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na Mbunge wa Kuteuliwa, Humphrey Polepole ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa.

Askofu Gwajima ndiye mwana CCM wa kwanza kutoka hadharani akiwa mbele ya madhabau ya Kanisa lake lililopo Ubungo, Dar es Salaam tatehe 25 Julai 2021 na kuwaambia waumini wake kuwa haungi mkono ujio wa chanjo na kwamba yeye na watu wake hawatachanja.

Matendo na matamshi ya Askofu Gwajina na wa Polepole, ni kinyume na msimamo wa chama chao, CCM akiwemo mwenyekiti wao, Rais Samia Suluhu Hassan.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021.

error: Content is protected !!