Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole arusha vijembe upinzani
Habari za Siasa

Polepole arusha vijembe upinzani

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameeleza kuwashangaa wapinzani kwa kudhani kampeni nzuri zinaweza kuwapa ushindi. Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

“Wapinzani miaka yote hudhani ushindi katika uchaguzi hutokana na kampeni nzuri, hapana! ushindi ni matokeo ya uwekezaji wa muda mrefu ndani ya miaka mitano mliyopewa dhamana,” amesema Polepole ambaye ni mbunge aliyeteuliwa na Rais John Magufuli.

Amesema, ushindi wa chama hicho katika Uchaguzi wa Urais, Ubunge, Udiwani na Uwilishi uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, umetokana na uwekezaji wa muda mrefu.

Akizungumza na wanachama wa CCM tarehe 23 Desemba 2020, jijini Mbeya, Polepole amesema uwekezaji huo umefanyika katika muhula wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli.

Katika uchaguzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Rais Magufuli (CCM) alipata kura 12.5,  Tundu Lissu (Chadema) alipata milioni 1.9.

Pia Polepole amesema, katika uchaguzi mkuu ujao (2025) CCM kinaweza kupata asilimia kubwa zaidi ya ile ya mwaka huu katika urais.

“Sifanyi utabiri, nafanya uchambuzi, kama tukiendelea na muelekeo wa hivi 2025 ni zaidi ya  asilimia 84,” amesema Polepole.

Amesema, ongezeko hilo linatokana na ushindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambapo CCM kimezoa wabunge, wawakilishi na madiwani wengi.

“Hatutakiwi kushuka chini ya asilimia 84 mwaka 2025, kwa sababu tukishuka wananchi watatushangaa.

“Watasema wabunge mliokuwa hamna tuliwapa,  kura za urais tukawaongeza, madiwani tukawaongeza na kodi tukaongeza zaidi. Kwa nini msifanye vizuri tukawapa zaidi ya asilimia 84,” amesema Polepole.

Hata hivyo, Polepole amesema, kazi hiyo haitakuwa rahisi kama wanachama wa CCM watabweteka wakijua wamepata kila kitu.

“Lakini kazi hiyo ni ngumu sana, kwa nini? Kwa sababu kila kitu tunacho na mnapokuwa na kila kitu ndipo mtu huwa una-relax unajuna umeshamaliza, umeshapata, umeshafika,” amesema Polepole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!