Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole ‘aota’ majimbo ya upinzani Kaskazini
Habari za Siasa

Polepole ‘aota’ majimbo ya upinzani Kaskazini

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema chama hicho kitayarudisha majimbo yote yaliyochukuliwa na vyama vya upinzani katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro utakapofanyika uchaguzi mkuu hapo 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vikao vya juu vya chama hicho vilivyopangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Jumanne, tarehe 25 Juni 2019, jijini Dar es Salaam.

Polepole amesema CCM ilipoteza majimbo kadhaa katika uchaguzi mkuu uliopita (mwaka 2015) mbele ya vyama vya upinzani kwa sababu ya migogoro iliyodhoofisha uimara wa CCM. Amesema majimbo hayo yatarudishwa katika uchaguzi mkuu wa 2020 kwa kuwa “kwa sasa hakuna migogoro.”

Amesema, walioanzisha migogoro ndani ya CCM walikuwa viongozi ambao wamejitafakari na kurudi CCM. Hakumtaja kiongozi yeyote.

“Wanasema NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) imeanza uandikishaji Kilimanjaro sababu ni kuwanyima haki wapigakura katika maeneo ngome ya chama cha Mbowe (Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema). Nani kakuambia ni ngome ya Mbowe, tizama wabunge wa 2010-15 CCM ilikuwa imetamalaki, na 2015 upinzani umeingia kwa sababu ya tofauti zetu,” amesema.

Uamuzi wa NEC kutangaza uandikishaji wapigakura mikoa ya Kilimanjaro na Arusha umelalamikiwa na upinzani kwasababu, tume imepanga kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi kiasi cha kuaminika watu wengi wenye sifa watakosa haki ya kuandikishwa kuwa wapigakura.

 “Hakuna kingine na tofauti hizo wengi walioziongoza wameshajitafakari (na) wamerudi CCM, sasa unasubiri nini? Alofanya uende upinzani yuko CCM. Nataka niseme bayana 2020 hakuna pale anayebaki, sijaona anayebakia pale,” amesema Polepole.

Katika uchaguzi wa mwaka 2015, majimbo matano kati ya saba katika mkoa wa Kilimanjaro yalichukuliwa na Chadema. NCCR-Mageuzi walichukua jimbo moja la Vunjo alikochaguliwa James Mbatia na CCM jimbo moja la Mwanga alikochaguliwa Profesa Jumanne Maghembe.

Majimbo matano waliyobeba wabunge wa Chadema ni Hai (Freeman Mbowe), Siha (Dk. Godwin Mollel), Moshi Mjini (Jaffary Michael), Same Mashariki (Nagenjwa Kaboyoka) na Rombo (Joseph Selasini).

Kwa upande wa mkoa wa Arusha wenye majimbo saba, Chadema ilishinda majimbo sita huku CCM ikishinda jimbo la saba la Ngorongoro kupitia William Tate Ole Nasha.

Majimbo waliyobeba Chadema ni Arumeru Magharibi (Gibson Ole Mesiyeki), Arumeru Mashariki (Joshua Nassari), Arusha Mjini (Godbless Lema), Karatu (Wille Qambalo), Longido (Onesmo Ole Nangole) na Monduli (Julius Kalanga).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!