August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polepole ajibu mapigo Chadema

Spread the love

MUDA mchache baada ya Baraza la Wazee Chadema kujitokeza kupinga kauli ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya kutaka Rais Magufuli awe Rais wa siku zote, Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uwenezi CCM amesema Rais huyo Mstaafu  hajafanya kosa kumsifia John Magufuli, Rais wa Tanzania na kuonesha hisia zake, anaandika Yasinta Francis.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliyoshawishi Rais Magufuli awe Rais wa siku zoteRais huyo mstaafu alinukuliwa  katika ibada ya Sikukuu ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaamakisema “Kama si matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote..laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa rais, ningeshauri Rais Dk. Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote”.

“Ni rais wetu mstaafu ni raia mwandamizi ana uhuru wa kuweka mawazo yake hadharani, anaikubali kasi ya chama cha mapinduzi chini ya mwenyekiti John  Magufuli. lakini nchi hii inaongozwa kwa katiba.

“Na rais wetu alishawaambia hataongeza hata dakika moja akimaliza muda ambao wananchi wamempa dhamana kwahiyo msianze kumzonga mzee wetu mzee Mwinyi, Ndio Mzee wetu tuliyenaye mwacheni aseme mambo ana uhuru wake wa kusema yake ya moyoni,” amesema Polepole.

Roderick Lutembeka, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Chadema Taifa katika tamko lake leo alimtaka Rais Magufuli kujitokeza na kuonesha msimamo wake katika suala hilo ambalo wamelitafsiri kuwa ni kutaka kujenga utayari wa wananchi kukubari kuwa na rais asiye na ukomo.

.

error: Content is protected !!