May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Plujim Kurejea tena Yanga?

Spread the love

HATIMAYE uongozi wa Klabu ya Yanga umeandikia barua ya kumuomba Hans Van De Plujim, aliyekuwa kocha kabla ya kujiuzulu afute maamuzi hayo na kurejea tena kuendelea kuinoa klabu hiyo, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Plujim alichukua maamuzi hayo baada ya kudaiwa kuwa uongozi wa Yanga ulikuwa katikamipango ya kufanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi lililokuwa chini ya kocha huku kocha mzambia George Lwandamila akitajwa kutakiwa kurithi mikoba yake.

Barua ya uongozi wa Yanga umeeleza kuwa, wanakiri kupokea barua ya Plujim kujiuzulu aliyoandika tarehe 22 Oktoba, mwaka huu.

“Tangu ulipojiunga na klabu ya Yanga Desemba mwaka 2014, umepata mafanikio makubwa na umeisaidia timu kushinda taji la Ligi Kuu ya Vodacom mara mbili mfululizo, ngao ya hisani pamoja na Kombe la Shirikisho (FA), kwa takwimu hizi uongozi wa klabu ya Yanga umekataa maombi yako ya kujiuzulu na kwa barua hii tunakuomba kurudi katika nafasi yako kama kocha mkuu wa Yanga kwa sasa,” imeeleza barua hiyo.

Lakini pia uongozi wa klabu hiyo haukuacha kumshukuru Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya hiyo kwa kuingilia kati kwa haraka kwenye jambo hilo kwa ajili ya mafanikio ya klabu.

Kujiuzulu kwa Plujim katika nafasi hiyo kulishangaza wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kiasi cha kuifikisha katika hatua ya makundi katika kombe la CAF kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 15.

error: Content is protected !!