Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo Pitso Mosimane katika mtihani wa kwanza kwa Al Ahly
Michezo

Pitso Mosimane katika mtihani wa kwanza kwa Al Ahly

Pitso Mosimane
Spread the love

KOCHA mpya wa klabu ya Al Ahly, Pitso Mosimane atakuwa na kibarua kigumu kesho kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Waydad Casablanca ambao watakuwa nyumbani nchini Morocco. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Waydad ambao wamemaliza msimu wa Ligi Kuu nchini Morocco bila taji hilo mara baada ya kushika nafasi ya pili kwa kutofautiana pointi moja dhidi ya mabingwa Raja Casablanca waliokuwa na pointi 60.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo mji wa Casablanca nchini humo, huku Pitso ambaye ni moja ya kocha bora barani Afrika atakuwa na kibarua kigumu kuwakabili Waydad ambao wanaonekana kuwa na kikosi bora kwa sasa.

Pitso anakwenda kukiongoza kikosi chake cha Al Ahly kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na timu hiyo tarehe 1 Oktoba, 2020, akitokea Mamelod Sundown inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza wa nusu fainali utachezwa kesho tarehe 17 Oktoba, 2020 na mchezo wa marudiano wa raundi ya pili utapigwa Cairo, Misri Ijumaa ya tarehe 6 Novemba, 2020.

Mashabiki wa klabu hiyo wana mategemeo makubwa na Pitso kufanya vizuri hasa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo hawajafanya vizuri kwa muda mrefu toka mwaka 2013 walipochukua taji hilo kwa mara ya mwisho.

Tayari kikosi cha Al Ahly kipo nchini Morocco kwa ajili ya mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mchezo wa mwisho kwa bao 1-0 dhidi ya Waydad nchini Morocco na marudiano kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani Afrika msimu wa 2016/17.

Mpaka sasa Pitso ameiongoza Al Ahly kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu nchini Misri na kufanikiwa kushinda michezo miwili na kwenda sare mechi moja na kufanikiwa kutoruhusu bao lolote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Vijana (U20) kwa Kagera Sugar FC

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20...

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

error: Content is protected !!