Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Michezo Pitso Mosimane aibwaga Mamelodi, atimkia Al Ahly
Michezo

Pitso Mosimane aibwaga Mamelodi, atimkia Al Ahly

Pitso Mosimane
Spread the love

ALIYEKUWA kocha mkuu wa klabu ya Mamelody Sundown inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini Pitso Mosimane ameachana na klabu hiyo hii leo 30 Octoba 2020 na kutimkia kwa vigogo wa soka la nchini Misri, Al Ahly. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kocha huyo tayari amekwisha kubaliana kujiunga na miamba ya soka nchini Misri klabu ya Al Ahly kwa mkataba wa miaka miwili mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu nchini Afrika kusini.

Katika taarifa yake aliyoitoa hii leo Pitso amemshukuru Rais wa klabu Mamelodi Dr Patrice Motsepe kwa ushilikiano aliyempa kwa kuwa asingeweza kupata hata nusu ya mafanikio aliyonayo sasa kama kocha na kubaliki kuondoka kwake kwenye timu licha ya kubakiza miaka mine kwenye mkataba wake.

Aidha amewaaga mashabiki wa timu hiyo ambao wiki iliyopita aliwapa taji la 10 la ubingwa wa Ligi Kuu.

Kwa upande wa klabu ya Mamelodi kupitia Rais wao walitoa taarifa ya kuthibitisha kuondoka kwa kocha huyo mara baada ya kupata ofa kutoka klabu ya Al Ahly.

Katika taarifa hiyo Motsepe ameeleza kuwa amepokea taarifa kutoka kwa kocha huyo juu ya kuondoka kwake kwa kuwa alikuwa anajua kila kinachoendelea katika mazungumzo kati ya Pitso na klabu ya Al Ahly.

Rasi huyo pia ameleza kujivunia mafanikio ya Pitso ndani ya Mamelodi kwa kuwa ni kocha mwenye mafanikio katika historia ya klabu hiyo na kuongezea kuwa wanatarajia kumtangaza kocha mpya hivi karibuni.

Pitso amedumu Mamelodi kwa miaka nane toka alipojiunga na klabu hiyo Desemba 2012, na kufanikiwa kutwaa mataji matano ya Ligi kuu nchini humo (Psl), na kutwaa mataji ya klabu bingwa na kombe la shirikisho barani Afrika mara moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Unamalizaje ligi kama hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

error: Content is protected !!