December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pingamizi 7 kina Mbowe latupwa, shahidi aliyekutwa na diary apeta

Spread the love

 

PINGAMIZI la utetezi dhidi ya kumkataa shahidi wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi wa pingamizi hilo, umetolewa leo Jumatano, tarehe 17 Novemba 2021 na Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo ya ndogo ndani ya kesi ya msingi ya makossa ya ugadidi ianyowakabili washtakiwa wote wanne.

Kutupwa kwa pingamizi hilo, kunafanya mapingamizi ya utetezi yaliyowekwa tangu kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo mwishoni mwa Agosti mwaka huu kufikia saba huku waliyoshinda yakiwa mawili pekee.

Miongoni mwa mapingamizi yaliyopitwa; ni uhalali wa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo, maelezo ya onyo ya mshitakiwa Adam Kasekwa yasipokelewe na hati iliyotumika kufungua kesi hiyo kuwa na makossa ya kisheria.

Jingine; ni hati ya ukamataji mali za washtakiwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya iliyowasilishwa mahakamani isipokelwe na lile lililohusu usahihi wa saini ya shahidi wa nne wa Jamhuri, Anita Mtaro (45), mfanyabiashara wa mbege, Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Upande wa utetezi, walitaka shahidi huyo asaini pembeni ili kulinganisha saini alizokuwa amesaini katika fomu zilizotumika kujaza vitu walivyokutwanavyo Kasekwa na Lingw’enya mara baada ya kukamatwa huko Rau Madukani.

Kuhusu pingamizi la saba, liliwekwa Ijumaa iliyopita, tarehe 12 Novemba 2021, baada ya upande wa utetezi kudai, shahidi huyo, askari polisi, Ricardo Msemwa kukytwa kizimbani akiwa na simu, kalamu na ‘diary’ (shajala).

Msemwa alikuwa akitoa ushahidi katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshitakiwa Mohamed Ling’wenya yasipokelewe mahakamani hapo.

Walidai, mtuhumiwa huyo hakuandikwa maelezo katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, tarehe 7 Agosti mwaka jana bali alisainishwa karatasi yenye maelezo yaliyodaiwa kuwa ya kwake katika Kituo cha Polisi cha Mbweni jijini humo.

Jaji Tiganga ambaye aliahirisha jana Jumanne kutoa uamuzi huo, leo Jumatano tarehe 17 Novemba 2021, ameutoa mbele ya mawakili wa pande zote na washtakiwa wenyewe ambao ni Mbowe, Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Amesema, baada ya pingamizi hilo kuwekwa kuwa shahidi huyo alikuwa na vifaa hivyo ambavyo alivitoa yeye mwenyewe akiwa kizimbani, Mahakama ikaona hakuwa akitumia simu yake basi Mahakama ikaona arudishiwe simu yake.

Jaji Tiganga amesema, baada ya hapo, Mahakama ikabakia na diary na kalamu. Hata hivyo, Mahakama ikawaelekeza mawakili wakafanye utafiti ili Jumatatu ya tarehe 15 Novemba 2021, waje waieleze wamepata nini kabla ya mahakama kutoa uamuzi wake.

Amesema, mawakili wa pande zote, walitoa hoja mbalimbali ikiwemo kurejea kesi kadhaa ambapo amezitaja baadhi kama Nanyaro vs Peniel, Edward Isack Shayo vs Jamhuri, Okumu vs Uganda, Goodluck Kyando vs Jamhuri ambapo amesema, zote zimetumika katika kutoa uamuzi huo.

Jaji Tiganga amesema, msingi wa hoja kwmaba shahidi hatakiwi kuwa na kitu chochote wakati Mahakama ikiendelea bila kuwa na kibali cha Mahakama, ukweli ni kwamba walimuona shahidi wakati hoja zingine za mawakili wa Serikali wakizitoa. Hakuna ushahidi kwamba alikuwa akirejea jambo lolote.

Jaji huyo amesema, utetezi walisema tungalie sheria na PGO ambapo inaruhusu askari polisi ambaye ni shahidi kuingia na diary kwa ruhusa ya Mahakama. Na kwamba anaweza kujikimbusha kwenye diary baada tu ya kuruhusiwa na Mahakama.

“Nakubalina na upande wa mashitaka kwamba shahidi anaruhusiwa kuingia na notebook kwenye kizimba cha Mahakama. Kwamba hakuna sheria ya moja kwa moja inakataza shahidi kuingia na notebook kwenye kizimba cha Mahakama,” amesema

Kuhusu hoja ya je, shahidi huyo ambaye ni askari polisi wa Oysterbay aliitumia diary hiyo wakati amesema, shahidi yeyote anapokuwa anaendelea kutoa ushahidi mahakamani ataruhisiwa kufanya ukumbusho.

Na kwamba wakati anaandika hiyo nyaraka alikuwa na kumbukumbu wakati huo. Na kwamba aliposoma andiko hilo lilikuwa sahihi.

Basi ukisoma PGO 282 (7) A & A na Sheria ya Ushahidi kifungu cha 168 1 na 2 shahidi hakatazwi kuingia na kitu chochote kwenye kizimba na kwamba kabla hajafanya marejeo ataomba ruhusa ya Mahakama.

Jaji Tiganga akigusia hoja ya kumwondoa kuwa shahidi, amesema sheria inasema ni shahidi ambaye hana uwezo wa kujibu maswali na kwamba iwe imesababishwa na umri mkubwa au mdogo.

Amesema, upande wa utetezi wameomba itumike hiyo ya mwisho ya ‘any other similar cause’. Mahakama imeombwa kurejea kwenye andiko ambalo Mr Kibatala alilirejea hapa Mahakamani akiwa ameichukua kutoka North Carolina, kwamba moja ya mambo kwao ni pale shahidi anakosa sifa ni kwa shahidi kukosa kuona umuhumimu wa kutoa ushahidi wake.

“Kwa sababu hiyo, sheria hiyo kwetu Tanzania hakuna. Mtobesya ameiomba mahakama ifanye kazi ya Bunge. Mahakama haiwezi kuongezea jambo hilo pamoja na kuomba kwamba Mahakama inaweza kuongezea sheria hiyo pale ambapo inaona kwamba kuna ulazima wa kufanya jambo hilo,” amesema Jaji Tiganga

Kuhusu kuikagua diary hiyo kuangalia imeandikwa nini, Jaji Tiganga amewataka wakili mmoja mmoja kutoka kila upande pamoja na ofisa wa mahakama kwenda kuikagua huku akitoa uamuzi kwamba, isipigwe picha yoyote.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!