July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda: Kuandika wosia sio uchuro

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Spread the love

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewataka wananchi kujijengea desturi ya kuandika wosia na kuorodhesha mali zao kabla ya kifo ili kuondoa migogoro katika familia. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Pinda ametoa wito huo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 25 ya Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), akisema kuandika wosio mapema sio kujichuria kifo.

Amesema wanawake ndio wahanga wakubwa katika mgawanyo wa mali za familia.

Akizungumzia changamoto na mafanikio ya TAWLA kwa miaka25, Mwenyekiti wa chama hicho, Aisha Bade amesema, “uwepo wao umewasaidia wanawake wengi”.

Bade amesema, TAWLA kimepiga hatua kubwa katika kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto, ambapo hadi sasa kuna wanachama zaidi ya 571 katika nchi nzima na kina wasaidizi wa kisheria 400.

Amesema, “hatua nyingine waliyopiga ni kuhamasisha jamii kwa nguvu zote na kuweza kuwafikia watu 15 milioni kwa kuwapatia vipeperushi na majarida mbalimbali ya kufundisha.

Amefafanua kuwa, hadi sasa wameshawasaidia wanawake zaidi ya milioni 5 katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Arusha na Dar es Salaam, ambapo wamewapatia msaada wa kisheria katika kupigania haki zao.

“Hatua nyingine tuliyopiga ni kuweza kutoa msaada wa kisheria kwa njia ya simu, pasipo malipo yoyote, na zaidi ya wanawake 15,000 walisaidiwa mwaka jana” amesema Bade.

Mbali na mafanikio mengi waliyopata,amesema kuna changamoto nyingi zinazowakabiri kutekeleza malengo yao, ambapo wameomba Serikali kuwaunga mkono.

Ameeleza changamoto hizo kuwa ni, serikali isaidie kuunda kitengo maalum cha kushughuliki masuala ya kifamilia, yakiwemo ya ndoa kutokana na kwamba kuna masuala mengine ya kindoa hayawezi kutatuliwa mahakamani, hivyo wanawake huumizwa zaidi.

Mfumo huru wa kufatilia masuala ya usawa, Serikali iongeze uwezo wa kutoa huduma na msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto na kuwapeleka washauri vyuoni ili kupata ujuzi zaidi wa kushauri wanawake.

Hata hivyo, baada ya kusomwa kwa risala hiyo, Pinda ameitaka TAWLA kuendelea kutoa msaada katika jamii ili kuisaidia serikali katika kutimiza malengo yake kwa wananchi.

“Serikali ipo tayari kuunga mkono safari yenu, na niwatoe wasiwasi kwamba mapendekezo yenu katika katiba inayopendekezwa yatapewa kipau mbele kutokana na juhudi mnazofanya,”amesema Pinda.

error: Content is protected !!