January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda “awakimbia” walemavu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Spread the love

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, “amewakimbia” walemavu kwa kutohudhuria kongamono lao la kimataifa lililojumuisha nchi tatu za Swedeni, Rwanda na Tanzania. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).

Mmoja wa wasanii waliotumbuiza katika kongamano hilo kutoka nchini Kenya, bila kujua kama Pinda hakuweza kuhudhuria badala yake amekilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwezeshaji na Uwekezaji), Injinia Christopher Chiza, amemsifu kabla ya kuimba.

“Kabla ya kuendelea na wimbo wangu, naomba nikushukuru wewe Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kuwa pamoja nasi leo, huku kwetu Kenya, viongozi wakubwa huwa hawaji kwenye shughuli zetu walemavu…ahsante sana,” amesema na kuwaduza washiriki.

Katika hotuba yake kwenye kongamano hilo lilifanyika viwanja vya Karem jee jijini Dar es Salaam, Chiza amesema Serikali ipo tayari kuunga mkono misaada inayotolewa na nchi za jirani.

Chiza amesema hayo baada ya kupokea risala iliyosomwa na mwakilishi wa mabaraza ya walemavu Tanzania, Atusajigwe Msokwe, ikiomba serikali iongeze vyuo vya kutoa ujuzi kwa waalimu wa walemavu na vifaa vya kufundishia.

Katika risala yao, walemavu hao wamesema pamoja na serikali kujitahidi kuelimisha jamii juu ya uonevu kwa walemavu, bado kuna matatizo yanayowakabili shuleni na hivyo kushindwa kupata elimu bora kutokana na miundombinu mibovu.

Wameeleza kuwa shule nyingi za walemavu hazina walimu wa kutosha, hakuna vifaa vya kufundishia walemavu wa ngozi (Albino), hivyo kukosa elimu bora kama watoto wengine.

“Hakuna wahudumu wa kutosha wa kuweza kutusaidia pindi tunapokuwa maeneo ya shule, kwa mfano tukiwa tunataka kwenda chooni, unakuta kina mlango mdogo na tundu dogo la kujisaidia, hivyo inatupelekea kuchafua mazingira,” amesema mmoja wa walemavu hao.

Kwamba, kupitia mashirika mbalimbali duniani ambayo yanawasaidia walemavu, wanafarijika na kujiona kuwa wapo sawa na watoto wengine majumbani.

Aidha, Waziri Chiza kwa niaba ya Pinda amewashukuru wafadhili hao kutoka Rwanda na Swedeni kwa ushirikiano waliuonyesha kwa Tanzania katika kuwasaidia walemavu hao.

error: Content is protected !!