June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda atia guu urais, ajivunia Tamisemi

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameshika fomu yake ya urais. Kulia ni mkewe, Tunu Pinda.

Spread the love

BAADA ya kutangaza kuanza mbio za urais kimyakimya akiwa jijini London Uingereza, hatimaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amejitokeza rasmi kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi, akisema hana tabia ya kujitangaza amefanya mambo makubwa kiasi gani kama walivyo wengine na kwamba kama angefanya hivyo, basi wangemkoma. Anaadika Dany Tibason … (endelea).

Akizungumza mjini Dodoma leo mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM ili kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, Pinda ametamba kuwa hakuna mtu anaijua vizuri Tanzania kama yeye.

Pinda amewasilia katika Ofisi za CCM Makao Makuu, akiambatana na mkewe, Tunu Pinda, baadhi ya wabunge kama Marha Malata, Dk. Dalali Kafumu, Dk.Pudensiana Kikwembe, pamoja na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.Didas Masaburi na wafusai wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema “hakuna mtu anayeijua vizuri Tanzania kama mimi, kwani nimekuwa kiongozi kuanzia awamu ya kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, awamu ya pili ya Ally Hassan Mwinyi, awamu ya tatu ya Benjamini Mkapa na sasa awamu ya nne ya Jakaya Kikwete. Kote huko nimekuwa nikitumikia Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Pinda amesema kwa sasa yeye ndiye Waziri Mkuu, kwamba Tamisemi kupitia Wakurugenzi na watendaji wengine wa halamshauri ndio watendaji na watekelezaji wakuu wa Bajeti ya Serikali.

Ametamba kuwa maendeleo yote yanayoonekana sasa hivi ni kazi yake ya kuwasimamia watendaji walioko chini yake wakiwemo mawaziri.

“Tumefukuza wakurugenzi na watendaji wengine wa halmashauri zaidi ya 2000 kutokana na ubadhirifu wa fedha lakini hata sasa Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amekiri kuwa hali si mbaya sana katika halmashauri kwa kupata hati safi.

“Lakini kama ningekuwa na tabia ya kujitangza kama walivyo wenzangu kwa kweli mngenikoma maana nimefanya mengi sana,”amesema Pinda.

Ameongeza kuwa, maendeleo yanayoonekana hayakuja hivi hivi ila ni mipango iliyopangwa ikiwemo ya kuanzisha Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano mitano ambapo hadi kufikia mwaka 2018, barabara zote nchini zitakuwa zimekamilika kwa kiwango cha lami na baada ya hapo wataendelea na vipaumbele vingine kwani haiwezekani vipaumbele vyote vikawa sawa.

Pinda amesema, Rais Kikwete amefanya kazi kubwa lakini anawashangaa baadhi ya watangaza nia kudai kuwa hakufanya kitu wakati Tanzania sasa imeondolewa katika orodha ya nchi masikini duniani na ni nchi ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

“Siwezi kueleza nini nitafanya nini kwani Ilani ya CCM haijatoka, lakini nawaahidi Watanzania wote kuwa nitatekeleza kwa vitendo Ilani ya chama changu kwani kila kitu kinakuwepo ndani yake.

“Lakini mambo machache ambayo ningependa kuyatekeleza ikiwa Mungu atanijalia kupita ni kuimarisha utawala bora na mazingira,”amesema Pinda

Amefafanua kuwa, suala la utawala bora ni muhimu ili kuharakisha maendeleo ya nchi na suala la Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (Takukuru), wataangalia namna ya kuipa meno ili kuwashughulikia wanaojihusisha na vitendo vya rushwa,  na kwamba baadhi yao walikuwa hawataki taasisi hiyo iingine kwenye Katiba mpya.

Pinda amesema, Takukuru ikipewa meno haitahitaji kibali kutoka kwa Waziri Mkuu ili kuwafikisha watu mahakamani ila wakikamilisha taratibu zao hakuna lingine zaidi ya kuwapeleka wahusika mahakamani.

“Awamu ya tano tunakwenda kwa wananchi wa hali ya chini yaani wakulima na wafugaji, kuhakikisha kuwa tunajenga viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao yao.

“Nimesimamia kilimo hadi kufikia tani za ziada milioni mbili za mahindi wakati zamani Tanzania ilikuwa inaagiza kutoka nje ya nchi,”amesema Pinda.

Aidha, amebainisha kuwa ikiwa kutakuwa na viwanda vingi itasaidia kuondoa umasikini zaidi kwa watu wa hali ya chini kwani kwa sasa wataalam wanasema licha ya uchumi kukua lakini wananchi wanaonekana bado masikini.

Kwa mujibu wa Pinda, ndio maana awamu ya tano inakuwa serikali ya kujenga viwanda kwa ajili ya wakulima na wafugaji.

Akizungumzia kuhusu magari ya kifahari aina ya Landcruiser VX8, Pinda amesema kwa sasa serikali inanunua magari yenye CC 3000 tu kwani, gari moja aina ya VX8 lina thamani ya zaidi ya Sh. 300 milioni, kiasi ambacho kingeweza kuunua magari mawili au matatu.

“Ugomvi wangu mkubwa ulikuwa kwa magari hayo na wataalam walitushauri kuwa gari lenye CC 3000 linatosha na ndio maana halmashauri nyingi wanatumia Landcruiser mkonga lakini kama tungeacha, watu wangejinunulia magari watakavyo lakini hili tumelithibi tayari,”amesema.

error: Content is protected !!