October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda atamani JPM ‘adumu’

Spread the love

MIZENGO Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne, ameeleza kutamani Rais John Magufuli adumu madarakani kwa zaidi ya miaka 10 ya Kikatiba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Pinda ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Desemba 2019, wakati akishiriki Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCMTaifa, jijini Mwanza.

Ameeleza kutamani Rais Magufuli, angezidisha hata miaka mitano baada ya ile 10 ya Kikatiba, na kwamba kikwazo ni muundo wa Katiba ya Jamhuri.

“Mimi Napata matumaini sana, miaka hii 10 uliyopewa itatupeleka pazuri sana. Ni kwa kuwa tu Katiba zenyewe ziko tight (zimebana), lakini kama si kwa sababu hiyo, Wallah ningezema mzee ungeongeza tena, piga kama mitano tu.

“Sasa najua hata mkijaribu kum – convince (kumshawishi), atawakatalia tu lakini nataka niseme, kwa namna ninavyoguswa na kazi kubwa unayoifanya. Ni matumaini yetu katika kipindi hiki, hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha unatupa kiongozi mwingine mzuri…,” amesema Waziri Pinda.

Amewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu kuunga mkono juhudi za za Rais Magufuli, katika kuliletea maendeleo taifa.

“Tunge mkono juhudi hizi, nchi hii ina uwezo mkubwa. Kama wote tutatenda kama ambavyo anataka tutende, nchi hii tutaruka kwa muda mchache sana,” amesema.

error: Content is protected !!