July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda ahimiza fursa za kibiashara Mbeya

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mizengo Pinda

Spread the love

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema Mkoa wa Mbeya unaweza kupaa kiuchumi kama utazingatia fursa za kibiashara ilizonazo na kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo na mifugo. Anaandika Mwandishi wetu (endelea)

Pinda ametoa kauli hiyo Jumatatu wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo.

“Nguvu kubwa mnayo katika biashara hasa kama mtajitahidi kutumia vema fursa kubwa ya uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo mliyonayo,”amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa mkoa wa Mbeya katika msimu wa 2013/2014 umeweza kuzalisha tani 4,159,907 za nafaka na kuuwezesha kuwa na ziada ya chakula ya tani 3,347,680.

Hata hivyo, amesema mkoa wa Mbeya bado una fursa nzuri ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na unaweza kuiwezesha nchi kuuza chakula katika masoko ya Afrika na Afrika ya Mashariki kama watajipanga vizuri.

“Kutokana na ukuaji wa kasi wa idadi ya watu ambao ni asilimia 2.7, mtu akichukua pato hilo la mkoa na kuligawanya kwa idadi ya watu anapata wastani wa pato la kila mwananchi kuwa ni sh. 1,420,427.

“Kipato hicho, ni sawa na shilingi 118,369 kwa mwezi au shilingi 3,946 kwa siku sawa na Dola za Kimarekani 2.3,” amefafanua.

error: Content is protected !!