June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pinda ahamasisha BRN

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Pinda

Spread the love

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ni ile yenye manufa makubwa na ya haraka kwa wananchi walio wengi. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Pinda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya mwaka wa kwanza ya utekelezaji wa mfumo wa BRN jijini Dar es Salaam.

“Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika kutambua sekta sita za mwanzo ambazo ni kilimo, elimu, nishati, uchukuzi, utafutaji rasilimali fedha na maji ambazo leo ndiyo tunapokea taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka wa kwanza,” amesema Pinda.

Pinda amesema vigezo hivyo pia vilitumika kuchagua mazingira ya biashara na huduma za afya kuziingiza kwenye utaratibu wa BRN.

“Serikali inaamini kwamba kuimarika kwa mazingira ya biashara, hasa biashara ndogondogo, kutatoa fursa za watu wengi zaidi kujiajiri na kuajiri na kuajiri wengine,”ameongeza Pinda.

Ametoa wito kwa watendaji wote kujifunza na kuutumia mfumo huo ili

waweze kufikia malengo waliyojiwekea kwa haraka zaidi.

“Mambo matatu yanayoupa mfumo huu uwezo mkubwa zaidi ni kupanga kipaumbele; kuwa na nidhamu na uwazi; na haya mambo yako ndani ya uwezo wa kila Mmoja wetu,”amesema.

Kwa mujibu wa Pinda, Serkali itaendelea kuchukulia utekelezaji wa mfumo wa BRN kama jambo la kipaumbele katika kutekeleza majukumu yake.

Anaongeza kuwa; “Haitoshi kwamba tumepata mafanikio haya katika mwaka mmoja. Ni lazima sasa tuazimie sote kuchukua kanuni hizi na kuzitumia katika kila eneo la maisha yetu.

“Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tumetoa mchango kamili kwa Taifa letu kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya
Taifa ya Maendeleo hadi mwaka 2015,” amesema.

Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau, Prof. Issa Omari amesema utoaji wa taarifa hiyo ni hatua mojawapo kati ya hatua nane za mfumo huo. Amewataka watendaji wanaotekeleza mfum huo wahakikishe wanafuata hatua zote nane.

Prof. Omari anasema kwamba jambo msingi katika utekelezaji wa BRN ni kubadilisha maisha ya wananchi na siyo tu kupima utendaji kazi wa mawaziri wa sekta husika.

“Kwa mfano katika sekta ya elimu, watu wanashangaa ufaulu kupanda haraka… lakini tuna shuhuda za utoro kupungua kwenye shule moja kutoka watoto 500 hadi sifuri…Hii ni kwa sababu tuliishirikisha jamii hadi ngazi ya chini,” amesema.

error: Content is protected !!