April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pigo Pwani, Katibu Chadema amfuata Sumaye

Casmir Mabina, Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani

Spread the love

MAZINGIRA ya demokrasia goigoi ndani ya Chama cha Demokrasia na Mamendeleo (Chadema), yamemkimbiza Casmir Mabina, Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Mabina ametangaza uamuzi huo leo tarehe 4 Desemba 2019, jijini Dar es Salaam, saa chache baada ya Fredrick Sumaye, aliyekuwa mwenyekiti wa kanda hiyo, kutangaza kujiondoa Chadema.

Ingawa hakueleza sababu za kujiuzulu wadhifa huo, Mabina amesema ameamua kujiuzulu kutokana na mazingira ya siasa yaliyokuwepo ndani ya Chadema.

“Kutokana na mazingira ya kisiasa yalivyo ndani ya Chadema, leo nimewasilisha barua yangu ya kujiuzulu. Kwamba kwa mazingira haya lazima nijiuzluzu,” ameeleza Mabina.

Mabina amesema, atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa Chadema.

“Nimeeleza nitabakia kuwa mwanachama wa kawaida katika chama change, kwenye tawi langu. Labda kama kutakuwa na mambo mengine yatakayojitokeza,” amesema Mabina

error: Content is protected !!