April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pigo lingine Chadema, Ndugai amvua ubunge Nassari

Joshua Nassari

Spread the love

SPIKA wa bunge Job Ndugai amemwandikia barua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Semistocles Kaijage kumtaarifu kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki linaloongozwa na Joshua Nasari Chadema,Jimbo hilo lipo wazi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Alisema Jimbo hilo lipo wazi kutokana mbunge huyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kitendo chake cha kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge mfululizo.

Alisema mikutano hiyo ni mkutano wa 12 wa tarehe 4-14 Desemba mwaka jana mkutano wa 13 wa tarehe 6-16 Novemba 2018 na mkutano wa 14 wa tarehe 29 January had tarehe 9 februari 2019.

error: Content is protected !!