May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pigo Chadema, yapoteza ‘kamanda’ wake

Spread the love

 

EMMANUEL Lukmai, alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Bagamoyo amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo tarehe 21 Februari 2021 na Hemed Ali,

Katibu wa Kanda ya Pwani, kwamba Lukmai amefikwa na umauti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akielezea ugonjwa wake, Hemed amesema Lukmai ambaye alikuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Bagamoyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, alipatwa na tatizo la kushindwa kupumua.

“Mwanachama mwandamizi na kiongozi mwenzetu aliyekipenda chama chetu kwa hali na mali, ameondoka akiwa anapigania uhai/afya yake katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa changamoto za upumuaji,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza:

”Hakika tumepata pengo kubwa katika ujenzi wa chama Bagamoyo na Pwani kwa ujumla. Niwasihi na kuwaomba kama ilivyo desturi yetu, tushirikiane kumsitiri kwa heshima kuu anayostahiki.” 

Hemedi amesema, familia ya marehemu inaendelea na taratibu za mazishi, na kwamba msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu – Kerege, Bagamoyo.

“Tuendelee kuchukua tahadhari zote kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19,” imeeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!