October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Picha ya JPM yamwingiza matatani Idriss Sultan

Idriss Sultan

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amemuagiza Mchekeshaji Idris Sultan, kuripoti katika Kituo cha Polisi, kwa madai kwamba amevuka mipaka yake ya kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makonda ametoa agizo hilo leo tarehe 30 Oktoba 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagram, nusu saa baada ya Idris kuandika ujumbe ulioambatana na picha ya Rais John Magufuli, iliyohaririwa.

“Naona mipaka ya kazi yako huijui. Nenda sasa hivi kituo chochote cha polisi uwambie Makonda kaniambia nije, utakuta ujumbe wako,” ameagiza Makonda.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Idris aliandika ujumbe ulioambatana na picha ya Rais Magufuli, akisema kwamba “kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani.”

Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe huo, ikiwa ni siku moja baada ya Rais Magufuli kusheherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

https://twitter.com/IdrisSultan/status/1189467531628765185

error: Content is protected !!