Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Peter Msechu awekewa puto tumboni
Habari Mchanganyiko

Peter Msechu awekewa puto tumboni

Spread the love

MSANII Peter Msechu amekuwa miongoni mwa watu waliopatiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni (intragastric balloon) katika hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumzia matibabu hayo leo tarehe 26 Januari 2023 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema, matibabu hayo ya kuwekewa puto tumboni yanasaidia kupunguza uzito kwa watu wenye uzito wa zaidi ya kilo 90 ambapo Msechu ana kilo 144.

Hospitali ya Muhimbili –
Mloganzila

Kwa upande wake msanii huyo mbali na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya nchini pamoja na viongozi wote wa Serikali wanaohusika na sekta hiyo, amewaambia Watanzania wategemee mabadiliko makubwa.

“Leo ni siku ya kipekee kwanza kiafya na maendeleo binafsi kama binadamu ambaye ninahitaji afya njema baada ya kupambana muda mrefu kwa mazoezi na diet lakini mwishowe naishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kutuletea huduma ya kuwekewa puto. Huduma hii inafanyika kwa uweledi mkubwa na mimi nipo rayari kupata puto langu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!