January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Peter Banda kutimka Simba

Spread the love

 

WINGA wa klabu ya Simba Peter Banda anatarajia kutimka ndani ya kikosi cha Simba mara baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Malawi ‘The Flames’ kitakachoshiriki michuano ya Kombe la mataifa Afrika (AFCON). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Michuano hiyo mikubwa barani Afrika itafanyika nchini Cameroon kuanzia Januari 2022.

Tayari baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi la Malawi wameshakwea ndege kuelekea nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuingia kwenye michuano hiyo.

Kwa sasa Banda yupo nchini ambapo muda mfupi ujao akiwa na kikosi cha Simba watashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kmc, mchezo unaopigwa kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Malawi zinaeleza kuwa Banda atanaondoka nchini siku ya jumapili ya tarehe 26 Desemba, 2021 kwenda kujiunga na wenzake nchini Saudi Arabia ambapo timu hiyo imekita kambi.

Kwenye michuano hiyo Malawi imepangwa kundi B, sambamba na timu za Senegal, Zimbabwe na Guinea.

error: Content is protected !!