Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Penzi la Kajala, Harmonize lavunjika tena!
Michezo

Penzi la Kajala, Harmonize lavunjika tena!

Spread the love

YAMKINI uhusiano kati ya Msanii wa Bongo Muvi, Kajala Masanja na wa Bongofleva Rajabu Abdul ‘Harmonize’, umevunjika.

Hatua hiyo inakuja baada ya jana tarehe 8 Disemba, 2022 Kajala kuchapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram unaoashiria kuwa wawili hao hawapo pamoja tena. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kajala ameandika hivi, “Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia.

“Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu. Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. I forgive my X and I’m ready for the next.#Nimekoma# emporary post” – @kajalafrida.
Ujumbe huo umezidi kuzua mjadala katika mitandao ya kijamii hasa ikizingatiwa Juni 25 mwaka huu, Harmonize alimvalisha pete Kajala.

Tukio hilo lililopewa jina la ‘Late lunch’ lilihudhuriwa na watu wachache ambao ni marafiki na ndugu wa wasanii hao.

Aidha, Harmonize alifikia hatua hiyo baada ya kuhaha kwa zaidi ya miezi kadhaa ya kumuomba msamaha Kajala ikiwamo kumnunulia magari mawili ya Range Rover pamoja na kubandika picha yake kwenye mbao za matangazo katika barabara kubwa.

Hata hivyo, kabla ya penzi lao kurejea upya, wawili hao walitengana baada ya kudumu kwenye uhusiano wa kwanza kwa muda wa miezi miwili kuanzia Februari hadi Aprili mwaka jana.

Tukio hilo lilizua taharuki baada ya Harmonize kuwashtaki Kajala na mwanaye Paula kwamba wamevujisha picha zake za utupu kutokana na madai ya Mkurugenzi huyo wa Konde Boy kumshawishi Paula ili wabanjuke kimapenzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!