KOCHA wa West Ham United Slaven Bilic, amesema winga wa klabu hiyo Dimit Payet 29 amekataa kucheza tena kwenye timu hiyo, kutokana na shinikizo la kutaka kuuzwa ingawa hawapo tayari kumuachia mchezaji huyo kwa sasa.
Payet ambaye alinunuliwa kutoka klabu ya Olympic Marseille inayo shiriki ligi nchini Ufaransa, kwa ada ya uhamisho Pauni Milioni 10 katika dirisha kubwa la usajiri amekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu hiyo katika msimu uliomalizika kiasi cha kuvutia klabu kubwa barani Ulaya kutaka kumsajili.
Licha ya kugoma kucheza kwa sasa, lakini Bilic amesema hawako tayari kumuuza mchezaji huyo katika kipindi hiki ingawa haitaji kucheza hapo kwa sasa.
“Tumeshasema hatuitaji kumuuza mchezaji wetu bora kwa sasa, lakini Payet hataki kucheza kwetu” amesema Bilic
Katika msimu wa kwanza aliocheza akiwa na West Ham United, Payet alifunga jumla ya mabao 12 na kuchaguliwa kuwania tuzo za mchezaji bora wa kulipwa wa mwaka, nchini England.
West Ham ambayo mpaka sasa inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu nchini England, inatarajia kuwakalibisha Crystal Palace katika mchezo wa ligi siku ya Jumamosi.
Leave a comment