August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Papa Francis: Hatutaruhusu wanawake kuongoza kanisa

Spread the love

PAPA Francis, kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani amesema haafikiani na suala la wanawake kuongoza kanisa katika nafasi za juu ikiwemo upadre na uaskofu, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kiongozi huyo ameeleza suala hilo baada ya kurejea kutoka mji wa Malmo nchini Sweden, alikoenda kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 500 ya kiprotestanti, mwaliko aliopewa na  kanisa la kilutheri.

Akiwa Sweden aliweza kukutana na Antje Jackelen, Askofu Mkuu mwanamke wa kilutheri, hali hiyo iliwafanya waandishi wahabari waliofika uwanja wa ndege wa Roma kuhoji endapo kanisa katoliki lina matarajio ya kuwapa nafasi wanawake ya kuwa upadre, ukadinali au uaskofu kwa siku zijazo.

Papa Francis amesema, “Utaratibu wa wananawake katika kanisa Katoliki uko sahihi, tutafuata mwelekeo huo ingawa wanawake wanaweza kufanya mambo mengine mazuri zaidi ya wanaume,”amesema Papa Francis.

Aidha, aliwataka waandishi wa habari kurejea katika waraka ulioandikwa na Papa Yohana Paulo wa II, mwaka 1994 ambapo waraka huo unapinga wanawake kushika nafasi juu za katika kanisa hilo huku akitolea mfano wa Yesu Kristu, mwana wa Mungu aliyeteua mitume wa kiume pekee.

“Waraka uliotolewa na Mtakataifu Yohane Paulo II unaendelea  kubaki hivyo,” amesisitiza.

Papa Frncis amekuwa Kiongozi wa aina yake katika kanisa katoliki ambapo misimamo yake imekuwa ikistaajabisha wengi hasa pale aliposema wazi kwamba hakuna sababu ya kuwatenga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja bali kuwaombea waachane na tabia hizo.

Kupitia kauli hiyo watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga) walimpongeza kwa kuamini utakuwa mwanzo wa kanisa hilo kuruhusu vitendo hivyo viovu kwa mujibu wa kanisa.

Hapo awali kanisa Katoliki lilikuwa katika mvutano juu ya zuio la wanawake kuwa mapadre na maaskofu ambapo baadhi ya makasisi walitaka kurushusiwa kuongoza misa, kitendo ambacho hakikubaliwa na baadhi ya waumini huku wengine wakidai ni vyema kuongozwa na wanawake kuliko wanaume mashoga.

Ingawa Papa Francis ametoa kauli tatanishi zaidi baada ya kusema, kama mtu ana nia ya dhati ya kumtafuta Mungu yeye ni nani hata amzuie.

“Mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema, mimi ni nani wa kuhoji suala hilo?” amesema.

error: Content is protected !!