Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Papa Francis atoa wito
Habari Mchanganyiko

Papa Francis atoa wito

Papa Francis, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani
Spread the love

PAPA Francis, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani amesema, dunia haiwezi kupuuza ubaguzi wa rangi na kutengwa kwa watu. Inaripoti Mitandao ya kimataifa …(endelea)

Pia, ametoa wito wa kusimamisha uharibifu akisema, si sahihi na haivumiliki kutenda vurugu na uharibifu.

“Hatuwezi kujitia upofu kuhusu ubaguzi na kutengwa, lakini si sahihi kuendesha vurugu na uharibifu,” amesema Papa Francis leo tarehe 3 Juni 2020 akieleza hisia zake kuhusu kinachoendelea nchini Marekani.

Akitumia lugha ya Kiingereza amesema, analiombea Mungu taifa hilo lirejee katika hali ya amani na umoja.

Pia, amesisitiza umuhimu wa kuwa pamoja na kufikia muafaka kuhusu kile kilichotendeka ndani ya taifa hilo.

Taarifa za mchana huu leo Jumatano zinaeleza, maandamano nchini humo yanazidi kushika kasi huku vitendo vya uporaji na vurugu vikipungua kwa kiasi kikubwa.

Taarifa zinaeleza, miji ya Houston, Texas kumekuwa na maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea. Maeneo mengine yameanzisha maandamano kupinga mauaji ya Floyd.

Houston, eneo ambalo Floyd atazikwa, meya wa jiji hilo, Sylvester Turner amewaambia waandamanaji “Floyd hakufa bure,” kwamba ameacha somo Marekani.

Waandamaji katika Miji ya Los Angeles, Philadelphia, Atlanta na Seattle wameendelea kuvutana na vyombo vya usalama huku kukiwa hakuna dalili ya kupoa kwa maandamano hayo.

Matumizi makubwa ya gesi na maji kuwasha yameripotiwa kwenye miji ya Seattle, Portland na Atlanta

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!