November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Papa Francis atembelea Iraq

Spread the love

 

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, amepanga ziara ya historia nchini Iraq, kuanzia leo Ijumaa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zinasema, inakadiriwa takribani wanajeshi 10,000 wa Iraq watalinda usalama wa kiongozi huyo nchini humo.

Hii itakuwa ziara ya kwanza rasmi ya Papa Francis (84), nchini humo na kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa gonjwa la Corona.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, katika ziara hiyo ya siku nne, Papa Francis anakusudia kuihakikishia jamii ya Kikristo inayopungua nchini Iraq usalama wao.

Amepanga kukutana na kufanya majadiliano na Kiongozi wa Waislamu wa dhehebu la Kishia anayeheshimiwa sana nchini Iraq, Ayatollah Mkuu Ali Sistani.

Aidha, Papa Francis atafanya sala huko Mosul na kuhudhuria misa katika uwanja wa michezo.

Anakwenda nchini humo, licha ya ongezeko jipya la maambukizi ya Covid-19 nchini Iraq na hofu dhidi ya usalama wake.

Hata hivyo, kuna hofu kuwa ziara hiyo ya kiongozi huyo wa Kikiristo ulimwenguni, yaweza kuwa chanzo kingine cha kuenea kwa virusi vya Corona.

Katika mkesha wa ziara yake, Papa Francis atatoa heshima zake kwa wale wote wanaoteseka kutokana na miaka mingi ya machafuko.

Anasema, amekwenda Iraq kama “msafiri wa amani,” na anayekwenda kuomba msamaha na maridhiano kutoka kwa Mungu baada ya miaka mingi ya vita na ugaidi.”

Alisema, “nakuja miongoni mwenu pia kama hujaji wa amani…kutafuta ushirika unaotokana na kuomba na kutembea pamoja. Ninakuja kama ndungu na dada zetu wa dini nyingine katika nyayo za Baba Abrahamu, ambaye anajiunga na familia moja ya Waislamu, Wayahudi na Wakristo.”

Muda mfupi baada ya shambulio la roketi dhidi ya kambi inayokaliwa na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq, Papa alisema, “Wakristo wa Iraq hawawezi kuvunjwa moyo kwa mara ya pili.”

Papa John Paul wa pili alifuta safari yake nchini Iraq mwisho wa mwaka 1999, baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati yake na aliyekuwa rais wa taifa hilo, Saddam Hussein.

Ndani ya miongo miwili tangu wakati huo, moja ya jamii ya zamani ya Wakristo duniani, imeshuhudia idadi yake ikipungua kutoka milioni 1.4 hadi karibu 250,000.

Baadhi ya waamini wa dini hiyo, wamekimbilia ughaibuni kwa kuhofia mashambulio kwa misingi ya kidini ambayo yamekumba Iraq tangu Marekani ilipoivamia kijeshi mwaka 2003 na kumuondoa madarakani Saddam.

Maelfu ya watu pia wamekimbia makazi yao baada ya wanamgambo wa Islamic State (IS) kuteka eneo la Kaskazini mwa Iraq mwaka 2014 na kuharibu makanisa ya kihistoria, kuchukua mali zao na kuwapa masharti ya kodi, kuachana na dini yao ama wauawe.

Watu nchini Iraq walikumbatia Ukristo Karne ya kwanza AD, lakini kwa sasa, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Wakristo waliosalia Iraq, ni chini ya 200,000 – wanaoishi katika Bonde la Ninawi na mkoa wa Kurdistan Kaskazini.

Karibu asilimia 67, ni Wakatoliki, ambao wamedumisha utamaduni wao lakini wanatambua mamlaka ya papa kuwa ni Roma.

Wakristo wengine, asilimia 20 ni waumini wa kanasa la Syriac ya Mashariki wanaaminiwa kuwa wa kale nchini Iraq; huku waliosalia Waorthodox wa Syriac, Wakatoliki wa Syriac, Wakatoliki wa Armenian, wengine ni Waanglikana na Waprotestanti.

Kutokana na sababu za kiusalama na uongezeka la maambukizi ya Covid-19, Papa Francis atadhibiti kuonekana hadharani.

error: Content is protected !!