Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Papa Francis atakiwa kujiuzuru
Kimataifa

Papa Francis atakiwa kujiuzuru

Spread the love

CARLO Maria Vigano, Mjumbe wa zamani wa Vatican amemtaka Papa Francis, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani kujiuzulu kufuatia kadhia inayoliandama kanisa hilo ya mapadri wake kutuhumiwa kuwafanyia ukatili wa kingono watoto wadogo. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wito huo umetolewa na Askofu Mstaafu Vigano ikiwa imepita siku moja tangu Papa Francis kuomba msamaha kwa Mungu kuhusu kadhia hiyo, alipotemebelea nchini Ireland.

Hivi karibuni Ripoti ya Washauri wa Mahakama ya Marekani ilidai kuwa, zaidi ya mapadri 300 waliohusika na unyanyasaji wa kingono waliwaharibu watoto 1,000 katika dayosisi sita za Pennsylvania katika kipindi cha miaka 70.

Katika tamko lake lenye kurasa kumi na moja, Askofu Mstaafu Vigano alikumbushia tukio la Papa Francis la kumuondolea adhabu Mc Carrick, Askofu wa zamani wa Washngton DC aliyopewa na Papa Benedicto wa kumi na sita kutokana na utovu wa nidhamu, licha ya uwepo wa ushahidi unaoonyesha tabia mbaya na utovu wa nidhamu aliyowafanyia baadhi ya waseminari na mapadri.

Vigano alisema mnamo mwaka 2013 alizungumza na Papa Francis binafsi kuhusu adhabu hiyo na jinsi Mc Carrick alivyowapotosha waseminari na mapadri wengi.

“Katika wakati huu mgumu kwa kanisa anapaswa akubali makosa yake na kwa kuzingatia kanuni ya kanisa ya kutovumilia kabisa makosa haya, Papa Francis anapaswa awe wa kwanza kutoa mfano kwa makadinali na maaskofu waliomkingia kifua Mc Carrick kwa kujiuzulu pamoja nao,” amesema.

Hata hivyo, Vatican haikutoa maoni na au kupinga juu ya madai hayo ya Askofu Mstaafu Vigano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!