Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Papa Francis ataka kuzikwa nje ya Vatican
Kimataifa

Papa Francis ataka kuzikwa nje ya Vatican

Spread the love

Papa Francis ameamua kurahisisha taratibu za mazishi ya papa kwa kuwa wa kwanza kuzikwa nje ya Vatican katika zaidi ya karne moja. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Papa Francis ambaye anatimiza umri wa miaka 87 siku ya Jumapili ijayo, alifichua mipango ya mazishi yake katika mahojiano na televisheni ya N+ ya Mexico jana Jumanne jioni.

Katika mahojiano na mwandishi wa mtandao huo wa Vatican, Valentina Alazraki, yaliyorekodiwa kabla ya papa kuongoza Ibada ya Misa katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Francis alionekana kupata ahueni kutokana na ugonjwa wa mkamba.

Francis alisema kutokana na imani yake kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu, ameamua kuzikwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Maggiore lililopo Roma, ambako huwa anaenda kusali kabla na baada ya kila safari yake ya nje.

Mapapa wengi wamezikwa chini ya Basilica ya Mtakatifu Petro.

Papa wa mwisho kuzikwa nje ya Vatican alikuwa Leo XIII, aliyefariki mwaka 1903 na kuzikwa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterani mjini Roma.

Francis amesema atakuwa tayari kujiuzulu – kama Benedict alivyofanya mwaka 2013 – ikiwa afya yake itakuwa mbaya sana, lakini pia anaamini kuwa kujiuzulu kwa papa kusiwe jambo la kawaida.

Alipoulizwa kuhusu afya yake, alisema: “Najisikia vizuri, najisikia vizuri”. Ugonjwa wa mkamba ulimlazimu Francis kughairi safari ya Dubai mwezi huu ili kuhudhuria mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28.

Alifanyiwa upasuaji mwezi Juni kurekebisha ngiri ya tumbo na inaonekana kuwa amepona kabisa kutokana na upasuaji huo.

Alisema anatarajia kufanya safari tatu mwaka ujao, kwenda mahali fulani huko Polynesia, Ubelgiji na nchi yake ya asili ya Argentina kwa ziara yake ya kwanza huko tangu kuchaguliwa kwake 2013.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!