Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Papa Francis alazwa hospitali kutokana na maambukizi ya mapafu
Kimataifa

Papa Francis alazwa hospitali kutokana na maambukizi ya mapafu

Papa Francis, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani
Spread the love

 

KIONGOZI wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis jana Jumatano amelazwa hospitali kutokana na maambukizi ya mapafu baada ya kukabiliwa na matatizo ya kupumua katika siku za hivi karibuni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Msemaji wa Vatican, Matteo Bruni amesema kwamba Papa mwenye umri wa miaka 86 hana Covid 19.

Aidha, amesema Papa Francis atakaa hospitali kwa siku kadhaa za matibabu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Francis kulazwa hospitali tangu alipokaa siku 10 katika hospitali ya Gemelli mwezi Julai mwaka wa 2021 na kufanyiwa upasuaji kwenye tumbo.

Maswali yameibuka kuhusu hali ya afya ya Francis na uwezo wake kusherehekea matukio mengi ya wiki takatifu ambayo inaanza mwishoni mwa wiki hii na Jumapili ya matawi.

1 Comment

  • TBC, TB, TBS, TIB BANK, TBL inawakaribisha wenye mashindano ya mapinduzi (work on talk “mapinduzi”) ya BANGO la Vifo VYA TB, kudhibitisha viwango vya Tabia, uhifadhi wa fedha bank, UJENZI wa BAR nchini Tanzania MTAWALIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!