August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Papa atembelea makahaba

Papa Francis

Spread the love

PAPA Francis Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani amekaa kwa zaidi ya saa moja na makahaba waishio nchini Italia ambao walisafirisha kutoka nchi mbalimbali duniani, anaandika Wolfram Mwalongo.

Papa mwenye umri wa miaka 79 amekua akikemea vitendo vya kusafirisha wanawake kutoka taifa moja kwenda lingine ili kuwatumikisha katika biashara za ngono.

Akiwa na wanawake 20 waishio katika moja ya jengo linalomilikiwa na Kanisa Katoliki katika Mji Mkuu wa Italia kiongozi huyo alizungumza na wananwake hao akitaka kujua namna walivyoingia biashara hiyo haramu.

Wanawake hao wenye umri unakadiriwa kuwa kati ya miaka 30 walitekwa na mwanamme mmoja. Miongoni mwao wapo wanaigeria saba, waromania sita na wanawake wanne kutoka Albania, huku wengine watatu katika kundi hilo wakitoka Italia, Tunisia na Ukraine.

Aidha, wamekiri sababu kubwa inayopelekea kwenda huko kuwa ni ajira ambapo wafanyabiashara Italia na nchi nyingine kutoka mataifa ya Ulaya huwachukua kwa kuwaahidi kuwapa kazi na wakifika huko hulazimishwa kufanya ukahaba.

Papa Francis amewatia moyo makahaba hao wenye nia ya kuachana na biashara hiyo, amewataka wawe “thabiti” wakati wanapoanza maisha mapya kwa usaidizi wa kituo cha Papa Yohana wa pili.

error: Content is protected !!