Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Panyabuku waanza kubaini TB
Habari Mchanganyiko

Panyabuku waanza kubaini TB

Spread the love

 

WIZARA ya Afya nchini Tanzania, imeanza kutumia teknolojia ya panyabuku, kubaini ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kwa sampuli za wagonjwa wenye dalili hizo. Anaripoti Mwadishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Hatua hiyo, inalenga kuongeza uwezo wa kutambua vimelea hivyo hasa pale ambapo njia zingine zinashindwa kubaini.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi ambaye alitembelea kitengo hicho cha Apopo, kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro na kupongeza mapinduzi ya wanasayansi, kuwawezesha panyabuku kunusa na kubaini vimelea vya sampuli za makohozi yanayoletwa kwa ajili ya vipimo.

Prof. Makubi ameelekeza ndani ya mwaka huu, huduma hiyo iweze kuzifikia zaidi ya hospitali 100 nchini.

“Nawapongeza sana watafiti wa SUA kwa hatua ambayo mmefikia, kituo hiki baada ya kukitembelea, tumeona kimekua kikifanya ugunduzi wa vimelea vya kifua kikuu kwa kutumia hawa panya.”

“Lakini pia, wameweza kuwafundisha na kusambaza hiyo teknolojia katika nchi mbalimbali kama vile Msumbiji na Ethiopia ambako wanafanya kazi ya kupima ugonjwa wa kifua kikuu, na kwenye nchi za Angola ambako wanafanyakazi ya kutambua mabomu ya ardhini,” amesema Prof. Makubi.

Amesema, panya hao, wana uwezo mkubwa wa kugundua vimelea vya kifua kikuu hata kwa mtu ambaye alifanya vipimo hospitalini kama vile vya hadubuni na mashine za kupima vinasaba na vipimo vingine.

Profesa Makubi amesena, vipimo vikatoa majibu kuwa hana TB, lakini panya hao wana uwezo wa kubaini vimelea ambavyo mashine za hospitalini zinaweza zisibaini.

Amesema, panya mmoja anauwezo wa kugundua kama sampuli ina vimelea vya kifua kikuu kwa muda wa sekunde moja, na hupima sampuli za makohozi 100 kwa dakika 20, hivyo teknolojia hiyo inaweza kutumika hata kwenye upimaji wa sampuli nyingi kutoka kwenye kundi kubwa la watu kwa muda mfupi.

Hata hivyo, Prof. Makubi alishuhudia panya ajulikanae kwa jina la Justine aliyeweza kupima sampuli 60 za makohozi ndani ya dakika tano na kugundua sampuli sita zenye vimelea vya kifua kikuu.

Mpaka sasa huduma hiyo inatolewa katika Hospitali 74 na kuweza kubaini wagonjwa 14,680 ambao hawakuweza kugundulika kwa njia za kawaida.

Hii imesaidia wagonjwa 8,119 kuanza matibabu ambayo yamezuia maambukizi ya kifua kikuu kwa wanachi 81,190 hadi 121,785 ambao wangeweza kuambukizwa kutokana na mgonjwa mmoja ambaye hajatibiwa anaweza kuambukiza ugonjwa huo kwa watu wa karibu naye 10 hadi 15 kwa mwaka.

Mganga Mkuu huyo, aliahidi kulifanyia kazi ombi la Mkuu wa Mradi wa kutambua Kifua Kikuu kupitia Panya Buku, Dk. Georgies Mgode la kuitambua teknolojia hiyo ya panya katika mwongozo wa kutibu kifua kikuu hapa nchini.

Dk. Mgode amesema, kuanzia mwaka 2007 mpaka Desemba 2020, mradi huo umeshapokea na kupima sampuli za makohozi 559,428 kutoka kwa wahisiwa wa kifua kikuu 315,476.

Amesema, wameongeza utambuzi wa wagonjwa wa kifua kikuu kwa asilimia 40 katika maeneo ya mradi.

“Huduma hii ikisambaa maeneo mengi nchini, basi Tanzania inaweza kuondokana na janga la ugonjwa huu kwani tayari Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma unatambulika duniani kuwa mfano katika mapambano dhidi ya kifua kikuu,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!