July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

“Panya Road” watingisha Tabata

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.

Spread the love

KUNDI la vijana waporaji maarufu kama “Panya Road” linadaiwa kuvamia eneo la Tabata jijini Dar es Salaam na kuwashambuli watu kwa mapanga na nondo kisha kuwapora fedha na simu katika mitaa ya Kimanga na Kisukuru. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Lucas Mkondya, alipotakiwa na MwanaHALISIOnline kuthibitisha tukio hilo, alikiri kuwa na taarifa hizo lakini akasema hawezi kuzungumza na mwandishi kwenye simu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, hakuweza kupatikana katika simu yake ya kiganjani.

Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, amesema lilitokea saa 11 jioni jana ambapo wananchi waliporwa mali zao kabla ya askari polisi waliokuwa doria kuzima tukio hilo.

“Hilo kundi lilikuwa vijana wengi wametusumbua sana maeneo ya Tabata na kuwapora watu vitu vyao, ukiwa mbishi unakatwa mapanga,”amesema shuhuda huyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, “Panya Road” hao walikuwa wakilipiza kisasi baada ya mwenzao kuuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kumuibia mteja simu katika klabu moja maarufu iliyoko maeneo ya Tabata.

error: Content is protected !!