Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Panya road watikisa Bunge
Habari za SiasaTangulizi

Panya road watikisa Bunge

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameiagiza serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti uhalifu unaoendelea kufanywa na vijana katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma na Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka tena matukio ya uporaji wa mali, kujeruhi na kusababisha vifo hususani kwa mkoa wa Dar es salaam ambapo wahalifu hao wanajiita panya road, Mara wamejipachika jina la ‘Watu kazi’.

Spika Tulia ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Septemba, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akitolea uamuzi hoja ya dharura iliyowasilishwa bungeni hapo na Mbunge wa viti maalumu, Bahati Ndingo (CCM).

Akitumia kanuni ya 54, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Ndingo alisimama na kumuomba Spika Tulia aahirishe bunge kwa muda ili kujadili suala la usalama wa raia.

“Jana mkoani Dar es salaam vijana wahalifu wanaojiita ‘Panya road’ wameendelea kuvamia makazi ya watu na wapita njia, pia wamesababisha mauti ya raia.

“Vikundi kama hivi vimeendelea nchini, mara wanajiita watu kazi, diwani mmoja wa hapa dodoma amevamiwa, baadhi ya wabunge hapa Dodoma wamevamiwa na vijana hawa… ninaomba kwa unyeti wake Bunge liahirishwe kwa muda ili kuishauri serikali hatua za kuchukua,” Ndingo alitoa hoja na kuungwa mkono na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli.

https://www.youtube.com/watch?v=MyV9PAYMDSQ

Kamoli naye alisimama kwa kanuni ya 54 (1) na kumuomba Spika kuahirishwa kwa bunge ili kujadili suala hilo.

Hata hivyo, Spika Tulia amesema licha ya kwamba kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 55, wangeweza kujadili lakini kwa namna lilivyo jambo hilo linaangukia katika kifungu cha 3 kanuni ya 55, fasili ya (1), (2) ambayo inaelekezwa jambo la aina hiyo kushughulikiwa na serikali kwa utaratibu wa kawaida.

“Lakini kwa namna limeshaathiri maisha ya watu, mali zao na jana tumezungumza athari zake namna zinavyoenda mbali, pamoja na serikali kushughgulikia katika utaaratibu wa wakaida ni kwamba tunaipa fursa serikali kushughulikia jambo hili kwa haraka.

“Sheria inatoa fursa wa serikali kuchukua hatua za haraka kwa sababu tulishapata hizo changamoto na serikali ikafanyia kazi na mambo yakaisha, hata hili ina uwezo wa kulimaliza, kanuni ya 55, masharti yake yananitaka kuielekeza serikali kuchukua hatua za haraka,” amesema.

Amesema hatua hizo sio kwa sababu wabunge wameathiriwa na mali zao bali pia wapo wananchi waliopata athari kwa kuumizwa na wengine kupoteza maisha yao.

“Kwa kuwa mambo haya hayajakidhi masharti ya kanuni ya 55, naagiza serikali ichukue utaratibu wake na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu yupo… mtalichukua kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua zile tunazozitarajia kutoka kwenu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!