Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, watuhumiwa 25 wa uhalifu wa kutumia silaha maarufu kama Panya Road. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi hilo, watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo leo Jumanne, tarehe 17 Mei 2022 na kusomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu Mkazi, Fadhili Luvinga.

“Kwa mara nyingine kundi lingine la wahalifu 25 ambao wengi wao ni vijana maarufu kama ”Panya road” waliokamatwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha. Walifikishwa mbele ya Hakimu Luvinga kusomewa mashtaka sita yanayowakabili,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, watuhumiwa hao walisomewa mashtaka na waendesha mashtaka wa Serikali, Wakili Michael Ng’hoboko, Avelina Ombock na Nancy Mushumbusi.

Wakiwasomea mashtaka hayo, mawakili hao wa Serikali walidai watuhumiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, tarehe 24 Aprili, 2022, 25 Aprili 2022 na 29 Aprili 2022, maeneo ya Gongo la Mboto, Kipunguni na Karakata jijini Dar es Salaam.

Waendesha Mashtaka walidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na waliomba tarehe kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

Hata hivyo, watuhumiwa wote walikana mashtaka waliyosomewa, kisha Hakimu Luvinga aliahirisha kesi zao hadi tarehe 26 Mei 2022 na 30 Mei 2022, ambap wapelekwa rumande kutokana na makosa wanayoshtakiwa kukosa dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *