Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Panga la Wakuu wa Mikoa, Wilaya laja
Habari za Siasa

Panga la Wakuu wa Mikoa, Wilaya laja

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema hivi karibuni atafanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi, ili safu yake ya uongozi ikamilike.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mama Samia ametoa ahadi hiyo leo Jumanne tarehe 6 Aprili 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati ana waapisha wakuu wa taasisi,  makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu, aliowateua  tarehe 4 Aprili mwaka huu.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amesema hayo wakati anazungumzia changamoto za Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ambayo inasimamia wateule hao wa rais.

“Najua TAMISEMI ni pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi na hiyo kazi itafuata hivi karibuni ili safu itimie na kazi iende kufanywa,” ameahidi Rais Samia.

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI,

Rais Samia amesema panga hilo litaanza na wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi ambao wanashindwa kutatua kero za wananchi.

 “Tumezoea tunao kwenda kwenye ziara mikoani, wiyalani tunapokelewa na mabango ya wananchi wakilalamikia kero mbalimbali, mabango mengine sio masuala ya kushughulikiwa ngazi za juu, ya kushughulikiwa chini,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutowanyamazisha wananchi wao kutoa kero zao, akisema kwamba akibaini atawachukulia hatua.

“Tunapokuja huko tukikuta bango ziwe issue (masuala)za kitaifa, ni za kushughulikia kule chini, nataka niseme bango moja aidha mkurugenzi, mkuu wa wilaya au mkoa umekwenda.

Na hii haina maana mkazuie watu kuandika kero zao sababu najua tunapokuja watu wakija na mabango mbiombio mnayakusanya na kuwanyuka watu kuwapeleka mnakokujua nyie ili wasiseme yanayowasibu,” amesema Rais Samia.

Tangu ameingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, Rais Samia amefanya panga pangua mara mbili, ya kwanza katika Baraza la Mawaziri na pili makatibu wakuu, manaibu katibu wakuu na wakuu wa taasisi za umma.

Mwanamama huyo aliingia madarakani kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli, kilichotokea katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, tarehe 17 Machi 2021.

Dk. Magufuli alifariki dunia kwa ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo, mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi 2021.

Tarehe 31 Machi 2021, Rais Samia alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, kufuatia hatua yake ya kumteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia aliwahamisha baadhi ya mawaziri pamoja na kuteua mawaziri wapya kadhaa.

Panga pangua ya pili ni ile aliyoifanya juzi Jumapili, kwa kuteua makatibu wakuu saba, manaibu katibu wakuu tisa na wakuu wa taasisi nane.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!