September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pambalu ajitosa uenyekiti BAVICHA

Bendera ya Chadema

Spread the love

JOHN Pambalu, Diwani Kata ya Butimba jijini Mwanza, ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha). Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Pambalu ambaye ni Makamu Mwenyekiti Bavicha, ametangaza nia hiyo leo tarehe 30 Novemba 2019, baada ya kurejesha fomu ya kugombea uenyekiti wa baraza hilo, kwenye Ofisi za Chadema, zilizoko jijini Dar es Salaam.

“Nimeamua kuutangazia umma wa Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba, nimetia nia ya kugombea uenyekiti wa Bavicha.  Uamuzi umekuja baada ya kujitafakari kwa ajili ya ukumbozi wetu,” amesema Pambalu.

Pambalu amesema amechukua hatua hiyo, ili kuwakomboa vijana na Watanzania kwa ujumla, kupitia Bavicha.

“Nimejipima nikaona katika siasa hizi za awamu ya tano, zinahitaji kijana jasiri dhidi ya siasa hizi za mabavu. Nina dhamira ya Kutatua changamoto za watanzania kupitia Bavicha, kwa kushirikiana na Chadema,” ameeleza Pambalu.

error: Content is protected !!