June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pakistani yakabidhi misaada Kinondoni

Spread the love

BONIFACE Jocob, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo amepokea msaada wa dawa za binadamu kutoka kwa Jeshi la Maji la Pakstani kupitia ubalozi wake nchini, anaandika Happyness Lidwino.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea msaada huo Jacob amesema, kikosi hicho kilicho na watu zaidi ya 300 kimetua nchini jana.

Amesema, kikosi hicho kimekuja na meli kubwa ya kivita kutoka nchini Pakistani kwa lengo la kufanya doria katika Bahari ya Hindi ambayo pia imepita nchini humu.

Meya Jacob amesema, meli hiyo ya kivita hufanya doria katika nchi zote ambamo Bahari ya Hindi imepita kwa lengo la kukomesha ujangili wa majini.

“Baada ya meli hiyo kutua jana ndipo uongozi wake ukaamua kutoa msaada kwa Watanzania kwa kutoa dawa za binadamu zinazotibu magojwa mbalimbali. Hatukuweza kujua gharama yake kwa muda huu lakini tutazisambaza katika hospitali zote za Wilaya ya Kinondoni,”amesema Jocob.

Hata hivyo, meya amesema mbali na kupewa msaada huo pia wamezungumza mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuimarisha ushirikiano kati ya Manispaa ya Kinondoni na nchi ya Pakstani.

“Nimefurahishwa sana na ujio wa wageni hao pia najisikia furaha kuwa wa kwanza kutembelewa na ubalozi huu na kupokea misaada hii kwani ni mwanzo wa ushirikiano mzuri baina yetu,” amesema Jacob.

Naye Amir Mohammad Khan, Balozi wa Pakistani amesema meli hiyo ina miaka mitatu sasa tangu ianze safari yake ya kutembea kwenye Bahari ya Hindi na hufanya hivyo kutoa misaada kila ifikapo kwenye nchi flani.

“Tumeshatoa misaada kwenye vituo vya kulelea yatima, shuleni na kwa watu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo tunakuwa tunatengeneza uhusiano mzuri kati ya nchi yetu na nchi hizo.

“Tuna ahidi kuongeza ushirikano baina ya Pakstani na Tanzania ili tuweze kusaidiana zaidi kwani kuynasiku pia nchi yetu itahitaji msaada kutoka kwenu,” amesema Khan.

error: Content is protected !!