June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Padri, wenzake watatu mbaroni kwa ubakaji, mauaji

Wanawake wakiandamana kudai haki kwa mtoto huyo

Spread the love

 

PADRE mmoja wa Kihindu (53) kutoka nchini India amejumuishwa katika kundi la watuhumiwa wanne wanaodaiwa kumbaka binti mmoja mwenye umri wa miaka tisa kisha kumuua. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Watuhumiwa wanadaiwa kutekeleza unyama huo tarehe 1 Agosti mwaka huu wakati mtooto huyo alipokwenda kuchota maji karibu na tanuru la kuchomea maiti.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini humo imesema kwamba padri huyo na wafanyakazi wengine watatu wa tanuru hilo, walimfanyia mtoto huyo kitendo hicho kisha mwili wake kuutumbukiza katika tanuru hilo la kuchomea maiti kama ilivyo desturi kwa wahindi.

Baada ya kumchoma moto, polisi walifika eneo la tukio na kufanya upelelezi wa kisayansi kupitia mabaki ya mwili wa mtoto huyo.

Aidha, mama wa mtoto huyo aliwaambia polisi kuwa baada ya watuhumiwa kutenda kosa hilo walimwambia kuwa iwapo atatoa taarifa polisi basi madaktari wangemtoa mtoto viungo na kuviuza.

error: Content is protected !!