May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pablo amgalagaza Nabi

Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Simba Pablo Franco amechaguliwa kuwa kocha bora wa LigI Kuu Tanzania Bara mwezi Machi mara baada ya kumshinda kocha wa Yanga Mohammed Nasredine Nabi pamoja na Francis Balaza wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali. Anaripoti kelvin Mwaipungu…(endelea)

Pablo ameshida tuzo hiyo mara baada ya kuchaguliwa na kamati ya tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ iliyokaa hivi karibuni.

Katika michezo waliocheza Simba ndani ya mwezi Machi, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Biashara United na pia ikaifunga Dodoma jiji mabao 2-0.

Kocha huyo alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, kwa kurithi mikoba ya Didier Gomes ambaye aliamua kuachana na timu hiyo kufutaia kupata matokeo mabaya kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Pablo anakuwa kocha wa sita kuzoa tuzo hiyo ya mwezi, toka kuanza kwa msimu huu huku makocha wengine waliotwaa tuzo hiyo ni Nabi ambaye alitwaa mara mbili mwezi wa Februari na Oktoba, Baraza mwezi Januari, Salum Mayanga Novemba, Malale Hamisi mwezi Septemba na Melis medo aliyekuwa anakinoa kikosi cha Coastal Union ambaye alitwaa tuzo hiyo Desemba.

error: Content is protected !!