August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

OUT yaanzisha shahada mpya

Spread the love

CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeanzisha programu mpya ya Shahada ya Uzamili iitwayo ‘Masters of Arts in Gender Studies’ itakayochukua miezi 18 kupatikana kwake,anaandika Happyness Lidwino.

Alexander Ndibalema, Mhadhiri Msaidizi wa OUT ameuambia mtandao huu leo kwamba, upo uhitaji mkubwa wa progamu hii katika jamii yetu kwa sasa.

“Tumeona kuna uelewa usio mpana kuhusiana na masuala ya jenda lakini hata hivyo kumekuwepo na uhitajiwa wa ngazi hii ya elimu katika masuala haya, chuo kimekamilisha taratibu zote na sasa tunaanza rasmi Aprili mwaka hu,” amesema Ndibalema.

Akifafanua programu hiyo amesema, lengu kubwa ni kuinua ufahamu wa masuala hayo kwa kuwa, jamii kwa sasa inatambua jenda ni kwa wanawake pekee.

“Ukizungumzia jenda watu wengi wanapeleka mawazo kuwa ni wanawake pekee lakini kumbe kuna mambo mengi yanawahusu wanaume. Tumeona kuwa namna bora ya kuinua ufahamu huu ni kuanzisha programu hii,” amesema.

Akizungumzia uelewa huo amesema, kila kundi lina matatizo na kuwepo kwa uelewa mpana upo uwezekano matatizo yaiyopo sasa yakatatuliwa na hatimaye kuwa na amani katika jamii.

“Huwezi kuwa na maendeleo kama hakuna amani katika jamii, lipo kundi la wanaume ambao wamekuwa wakinyanyaswa na wamekuwa wakishindwa kujiamini na kuelezea masaibu yanayowakuta. Programu hii itakuwa njia nzuri ya kuweka usawa kwenye jamii yetu.”

Hata hivyo ameeleza kwamba, yapo mambo ambayo yatabaki kuwa ya mwanamke na mwanaume pekee kwa namna alivyoumba Mungu lakini yale ambayo yanayokana na ufahamu mbaya, programu hii itakuwa msaada mkubwa.

Akitaja malengo ya program hiyo amesema ni pamoja na kuisaidia jamii kuelewa kuhusu masuala ya jenda, kufanya tafiti kuhusu masuala ya ya jenda na hatimaye kuyatatua kabla ya kuwa na athari zaidi, kuleta usawa katika jamii na kuongeza mawasiliano.

Ndibalema amesema kwamba, zipo njia mbili ambazo programu hii inaendeshwa moja ikiwa ni ya mwanachuo kuhudhuria darasani moja kwa moja na ya pili ni kwa kutumia njia ya  mtandao yaani online.

Amesema, mchanganuo wa namna ya kupatikana kwa shahada hiyo umewekwa vizuri kwenye mtandao wa chuo hicho “taarifa zetu zinapatikana vizuri hata kwenye mtandao wetu wa chuo www.out.ac.tz.”

error: Content is protected !!