July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Othuman: Viongozi wanaapa kulinda katiba yenye tatizo

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othuman Masoud Othuman

Spread the love

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othuman Masoud Othuman amesema, Katiba ya sasa ya Tanzania haitoi mwelekeo wa Taifa unakwenda wapi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Othuman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo amesema hayo leo Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021, alipozungumza wanachama wa chama hicho Jimbo la Mbagala.

“Katiba ndio dira yetu ya kuongoza nchi. Katiba tuliyonayo sasa haitupi hata uelekeo tunakwenda wapi. Hivyo tunakila sababu ya kupata Katiba Mpya.”

“Viongozi wanaapa kuilinda Katiba na Katiba yenyewe hii ya 1977 ni tatizo, maana yake watu wanaapa kulinda tatizo. Lazima tubadilishe katiba na tutengeneze katiba itakayotupa direction,” amesema Othuman.

Kuhusu uchaguzi amesema, ndio msingi wa uwajibikaji, “hakuna namna zaidi ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itawapa fursa wananchi kuchagua viongozi wawapendao kwa uhuru na haki.”

“Tunapozungumza uchaguzi hatuzungumzi uchaguzi kama swala la kisiasa uchaguzi ni fursa ya kuwapa wananchi kuchagua viongozi wa kutuwakilisha na kuwapima viongozi hao kama wamekidhi maagizo ya wananchi waliowapa mamlaka baada ya miaka mitano,” amesema

“Kiongozi ni mtu ambaye ananidhamu, anakubalika na anaaminika na umma. Hivyo tunavyo zungumza nchi hii tunahitaji kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi maana yake tunahitaji wananchi wawapate viongozi wenye kuwajibika na kuwatumikia Watanzania kwa weledi mkubwa.”

error: Content is protected !!